SlideShare a Scribd company logo
1 of 6
Download to read offline
1
WARAKA WA IKULU TAKATIFU KWA JOHN MAGUFULI, NA EDWARD
LOWASA NA HATMA YA TANZANIA
Na Prof Handley Mpoki Mafwenga
Ph.D (finance -COU), MSc (finance -Strathclyde), MBA (Mg.Eco -ESAMI/MsM), LLM
(taxation- UDSM), LLB (Tudarco), PGD tax mgt (IFM), AD tax mgt (IFM)]
Zamani nikiwa na umri mdogo nilifahamishwa kuwa ukiangalia sana Mwezi utaona
Nabii Elia amekalia kiti na amevaa taji, kainama anasikitikia Dunia. Dunia iliyojaa Chuki,
Dhiki,Dhambi na Damu ya Uasi wa kiroho. Nikawa naona ni kweli. Katika utu uzima
wangu tarehe 7 Septemba, 2015 ghafla naangalia Mwezi naona picha ya John
Magufuli, amekalia kiti, kashika Katiba ya Tanzania. Pembeni ya kiti kuna maneno
yameandikwa “Ikulu Takatifu” yamezungukwa na maua ya rangi ya kijani na njano;
picha ya nembo ya Taifa al-maarufu Adam na Eva na Bendera ya Taifa vimepamba
kofia yake. Aidha, kuna imani kuwa, Mawingu hutoa maumbo au picha
mbalimbali,mfano ukiliona umbo la samaki ni dalili ya neema kwako; umbo linaloonesha
tendo la ndoa ukiliona ni Uchuro hapo kuna kifo au nuksi kubwa; lakini umbo la sura ya
mtu ni kiashiria cha mateso na misukosuko ya kutafuta mafanikio bila kuyapata kwa mtu
huyo. Naliangalia wingu naona picha ya Edward Lowasa, ina maneno ya Kiingereza
No!, No! No! na mengine yakiwa “Ahsante Sana Watanzania, Mungu yu pamoja nami”.
Ghafla nazimia namuona Mwalimu Nyerere ameongozana na Wavuta kiko maarufu
Sebastian Kinyondo na Kamanda Abdalah Natepe wanavuta kiko zao zinatoa harufu ya
udi wanapiga kelele “Tunafukuza harufu ya chuki, damu, ufisadi, na kuilinda Ikulu”.
Wananipa Waraka nimpe John Magufuli, Edward Lowasa, na Watanzania usemao;
Watanzania wangu, hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa ndiyo wamiliki wa Ikulu kuliko
Wagombea wenu? Na kuwa radhi yangu inakaa ndani yenu?. Kama mtu akiiharibu
Ikulu kwa kumchagua Mgombea fisadi Mungu atamharibu mtu huyo, kwa maana Ikulu
ni mahala patakatifu, na ni miliki ya Taifa lenu. Wagombea wote ni halali, bali si wote
watakaoijenga hadhi ya Ikulu kwani John, na Edward wana karama tofauti lakini
Tanzania ni ileile.
Ikulu ilijengwa na Wajerumani mwaka 1891 na Gavana Chakosi Dikwe na kutumika
kama ngome yake, hadhi na siri zake zingali zinakumbukwa huku Kuzimu. Damu za
Askari walioiharibu Ikulu wakati wa vita kuu ya kwanza ya dunia inawalilia Wanangu
mlio hai. Jasho la Gavana wa kwanza wa kijerumani ndugu Horrace Byatt
aliyeboresha Ikulu Mwaka 1919 lingali linalowesha Sanda za Askari hao na kufuta
damu zao kila siku. Byatt analia na ananiuliza “Mwalimu Watanzania wanajua kuwa
baada ya mimi kuingia madarakani nililazimika kukaa katika makazi ya muda kwenye
ofisi zao za wizara ya Afya ili Ikulu iwe Mahala patakatifu?”. Kama mnavyofahamu,
2
Tanganyika ilikuwa chini ya utawala wa Ukoloni wa Waingereza na hapo ngome hiyo
(state house) iliitwa Government House na ilijengwa tena mwaka 1922 ambapo gavana
wa Kiswahili Sir Unapima Mkali aliyechukua utawala anawalilia Watanzania wasipoteze
hadhi ya Ikulu. Ndugu J. H Sinclair - Mtaalam wa majengo wakati wa ukoloni aliyetia
nakshi za jengo hilo anawaomba mboreshe Ikulu kwa dhana ya kuchagua Rais safi na
alinde Uadilifu. Ikulu maana yake ni Itetemia lenye asili ya Kinyamwezi hasa enzi za
mtemi Milambo, Makao Makuu ya ngome ya milambo yenye Uadilifu na hadhi paliitwa
kwikulu, ndio neno ikulu likatoholewa.
Edward kichwa chake chenye mvi ni taji ya utukufu wa Mashabiki wa siasa wasio na
weledi wa uchambuzi, lakini kikionekana katika njia ya haki kitalinda hadhi ya Ikulu na
nje ya njia ya haki ni laana ya Watanzania karne na karne zijazo. Ushujaa wa
uchapakazi na Uadilifu wa John ni Lulu ya Utulivu na Ushindi wa CCM unaozidi ustawi
wa Ngome ya UKAWA yenye karama nyingi zinazojumuisha kuwapoteza Prof Haruna
na Padre Mstahafu Wilbroad.
Kijana wangu Edward, unafahamu kuwa amdhihakiye Maskini humsuta Muumba wake,
unapoongelea Umaskini katika safari ya Ikulu uwe makini, ukifika Ikulu uwe radhi
kugawa nusu ya Mali zako kuwapa Maskini; na ujue kuwa changamoto ya Watanzania
ni uwezo wa kugawanya rasilimali zao lukuki, Ugawanyaji wa Mapato yao na
Uimarishaji wa Uchumi endelevu; dhana ya Umaskini ni Matokeo na siyo chanzo cha
Changamoto; aidha, ujue kuwa ajitengaye na CCM hutafuta matakwa yake mwenyewe
kwenda Ikulu; je una msingi imara wa muundo wa kichama kuenzi “Utatu wa Elimu”
yaani “Elimu, Elimu,Elimu” unaoenzi Azimio langu la Musoma?. Mwanangu Edward
nakutakia heri iliyo na nuru kuenzi Elimu maana kumbuka niliwaachia Imani kuwa
“Elimu ni Ufunguo wa Maisha”.
Kijana wangu John moyo wako umechangamka na ni dawa nzuri ya kukimbilia Ikulu;
hekima ipo machoni pako kwani una Ufahamu, isipokuwa uhamasike sana ndani ya
Kampeni, hujafika bado Ikulu,usishibe kabla hujala, usioge hujavua nguo; ongeza kasi
Ikulu inakukaribia. Tanzania yangu unataka iwe ya Uchumi wa viwanda utakaolinda
utajiri wa Mafuta na Gesi ukifungamanishwa na Sekta zingine ili zisije zikafa kwa
kukosa nguvu kazi itakayoweza kukimbilia kwenye Mafuta na Gesi, watakakolipwa
ujira zaidi na kuacha Sekta zingine kama vile Kilimo. John ndoto zako za kuboresha
Ujasilia-Mali ndani ya Uchumi wa viwanda ni wazi utapunguza Umaskini na Kuweka
Maendeleo ya Uchumi endelevu; utapunguza gharama za Uzalishaji na kupanua uwezo
wa Wananchi kulipa kodi. Lakini nakutakia heri katika jitihada za kufufua viwanda na
Ikulu ipo ndani ya mboni zako. Wewe ni Mkemia hapana shaka Viwanda vya mbolea
vitapata mtu, uhifadhi wa mazingira utaboreka na ukiwa Mwanahisabati Tanzania
itafanya kazi ki-Mahesabu. Ukiwa Ikulu anzisha Mifuko miwili ya Hifadhi ya Mapato ya
Mafuta na Gesi; mmoja wa kuimarisha Mapato dhidi ya Mnyumbo wa Uchumi
(Stalization Fund), na mwingine wa Uhifadhi wa Mapato kwa Vizazi vijavyo (Saving
Fund) ili uchumi wa viwanda uwe endelevu; hiyo iwe sambamba na Uadilifu wa
Matumizi ya Mapato..
Nimetambua kuwa kuna vyama vinanipa tabu huku Kuzimu;ACT ni watu wasio na
nguvu, lakini hujiwekea Hazina ya kisiasa wakati wa Heri ya Ikulu; NLD ni watu dhaifu
lakini hujibanza ndani ya mabawa ya UKAWA huo ni ulaghai wa kisiasa; CHADEMA na
CUF hawana Wafalme zao Wilboad na Haruna Ngunyuru waliozama chini ya kivuli
3
kinachoficha demokrasia, lakini vyama hivyo vinakodi Wafalme huku wakienda pamoja
vikosi vikosi ndani ya UKAWA; CCM hushika ubora wa Ilani yake wakimiliki Ikulu ya
Kivukoni, wakifurahia Upendo kwa nyimbo na lugha zilizojaa Mithali. Vyama hivi
huwachanganya Wananchi hawajui mwelekeo na Dira ya Uchaguzi Mkuu.
Kijana wangu John, nia yako ya kushughulikia maovu kwa moyo ni yako kama
Mwanadamu, jawabu la ulimi wako wenye Upako hutoka kwetu huku Kuzimu na kwa
Mungu. Mkabidhi Mungu Sera na Mawazo yako yatathibitika. Ulimi huo ni kama fedha
yenye thamani ndani ya soko la ndani na la nje linalopambana na myumbo wa uchumi;
fedha itakayofanikisha afya, elimu, maji, umeme na miundombinu laini na migumu, ili
Ikulu ithibitike. Matunda yangu na akina Rashid Kawawa, Oscar Kambona, Job Lusinde,
Amir Jamar, Nsilo Swai, Tewa Said Tewa, Chief Abdalah Fundikila, Dereck Bryceson,
Paul Bomani, Sir Ernest Vasseey, Sir George Kahama, Chief Abdalah Fundikira, Chifu
Lukumbuzya, Chief Adam Sapi Mkwawa, Mwami Theresia Ntare na wengine hupita
thamani ya dhahabu na vito ndiyo maana Ikulu ililinda Haki. Ukifuata nyendo zangu ni
mwanzo wa mwendelezo wa hekima na utakatifu utakaoongeza Ufahamu wako.
Mungu amewachukua Mashujaa wangu wote, wachache waliobaki watumieni; Mimi
nilipata mateso ya Watanzania na fimbo yangu hadi mkaniita “Musa” na kwavile
niliwatoa kwenye bwawa la mateso ya Kikoloni; Mungu aliniongoza katika giza wala si
katika nuru nilipokuwa Ikulu; nilichakaa nyama yangu na ngozi yangu; hadi nikafariki
mapema kuliko Nelson Mandela kwa kuwapenda Watanzania kubeba mzigo wa Ikulu.
Wanangu Watanzania; mmegeuza njia zangu zenye neema, mnararua rarua Sanda
yangu; mmenifanya mkiwa huku Butiama kwa ushabiki wa kisiasa, uliokosa tija ya fikra
na uchambuzi wa kina. Kumbukeni msiba wangu mlipolia mimi niliililia Ikulu, na Ikulu
ilinililia “Baba yangu, Baba yangu wa Taifa Mbona Unaniacha?” nami nikatamka
“Unyerere Umekwisha” nikakata roho.
Macho yangu yanatoa machozi hayakomi, ningali naililia Ikulu yangu; babu na bibi zenu
waliowarithisha Ikulu wanalia, watoto zenu waliowakopesha Ikulu ambao ni samani ya
Tanzania wataomboleza kama mtachagua Rais kwa ushabiki wa kisiasa. Wanangu
John na Edward, urithi wenu umegeuka kuwa mali ya Wageni na utajiri kuwa mali ya
Mafisadi. Watanzania wangu wamekuwa yatima walionyang’anywa urithi wao. Ondoeni
pepo la unyonyaji wa rasilimali zetu ili mlinde ushindani wa Wawekezaji wa nje na wa
ndani katika Mnyororo wa Thamani wa Uwekezaji; kumbukeni, Kiatu cha Mwanangu
Jakaya Kikwete kiliisha sori kulinda hadhi ya Ikulu, aliwatafutia Neema ndani na nje ya
nchi; Watanzania walio wengi hamkumsaidia, kazi yenu ikawa kulalama badala ya
kufanya kazi, mkitaka akae Msoga aende Ikulu kila siku mithiri ya Mfanyakazi wa
kawaida; mkatenganisha Ikulu na Urais kwa kupigwa upofu wa fikra mkilinganisha
gharama za Ikulu na za kununua bamia. Lakini mmesahau Yesu Kristo, Mtume
Mohammad (S.A.W), Nabii Musa na wengine hawakutulia kuwaletea Waja wa Mola
Neema na Ukombozi; yu heri Rais Jakaya Kikwete aliyeenzi Mila na Desturi ya ki-
Afrika kuwa Muwindaji (Mfwimi) kwa kuwapa Neema na Ukombozi wa ki-Uchumi.
Watanzania wangu, Albino mmewafanya wanyama¸ Binti Kabula Nkalango, Said
Abdalah, Nainana Daud,, Rukia Halfan na Fatma Halfan damu zao na viungo vyao
vingali vinavuja damu; Wauaji waliohukumiwa kunyogwa; Joseph Lugala,, Masumbuko
Madata, Emmanuel Masangwa, Charles Masangwa, Nchenyewe Kisiwa, Sayi Gamaya,
Mboje Mawe, Sayi Matizi, na Kazimir Mashauri roho zao zinatuchefua huku Kuzimu;
4
Chozi la Peter Kayanza Pinda halijakauka katika Sanda zetu. Vijana wangu John na
Edward mnapokwenda Ikulu zibeni Chemchem ya damu za Albino anzeni alipomalizia
Mhe Jakaya.
Mama zenu wamekuwa kama wajane mbali ya Mwanangu Jakaya Kikwete kuwajali
kwa hali na mali kwa mfano ameteua Wanawake wengi kuwa Majaji, hii ni kuenzi kazi
yetu ya tarehe 1 Septemba, 1970 ambapo Tanzania ilikuwa Nchi ya kwanza Afrika
Mashariki kuteua Hakimu Mkaazi Mwanamke; tulikuwa na uchache wa Mahakimu
Wakazi wakiwa 44 tu kati yao watatu wa-Nigeria, watano wa-Malawi na 36 wa-
Tanzania. Jaji Mkuu wa kwanza alikuwa Jaji Said aliyeteuliwa 1971 na Jaji Mkuu wa
kwanza wa Mhakama ya Rufaa ya Afrika Mashariki alikuwa Raia wa Tanzania; Ahsante
Jakaya Kikwete umetusetiri huku kuzimu akina mama wanakuombea maisha marefu
kwani wanaamini majaji wanawake watalinda Utawala wa Sheria mithiri ya binti wa
Faraoh aliyelinda Utawala wa Sheria dhidi ya Nabii Musa ndani ya nyumba ya Faraoh
baada ya kuokotwa baharini.
Nyuso za vikongwe hazipewi heshima huitwa Wachawi utafikiri nyie hamtazeeka,
mlidiriki kuchoma nyumba zao zaidi ya 20 wakati mnajua Katiba niliowaachia inazuia
Mauwaji,Ukandamizaji na Utesaji ambacho ni kinyume hata cha Sheria ya Makosa ya
Jinai na Sheria ya Uchawi ya Mwaka 1928; damu za waliouwawa kwa imani za Uchawi
Agripina Thomas, Anamaria Theda, Monica Spron wote wa Kagera, Amana Shawishi
wa Mwanza, Lyatoga Venance wa Makongoro Nansio, Cheupe Mwananzyuni wa
Rukwa na Frank Mwasha wa Nzega zinaililia Ikulu na Upendo kwa Watanzania;
Mabinti zenu wanabakwa na kukatizwa masomo, mabikra ni wa kuhesabu. Watoto wa
kiume hulawitiwa kinyume na Kifungu Na 156(1) cha Sheria ya Makosa ya Jinai. Roho
zetu zinamuombolezea mtoto wa miaka 13 wa Sumbawanga aliyetelekezwa na mama
yake muuza bia bar mjini Mbeya, mtoto aliyefiwa na baba yake akiwa na miaka saba
aliyelawitiwa kwa siku tatu na baba wa miaka 51 aliyekuwa akifanya kazi Kampuni ya
Majembe Auction Mart Sumbawanga kwavile mtoto aliishi katika mazingira magumu;
Aidha, Wakulima na Wafugaji mnauwana mashamba na mifugo imekuwa bora kuliko
roho zenu.
Enzi zangu moja ya Madhumuni ya Mwongozo wa TANU wa 1971 ilikuwa kulinda
maslahi ya Wananchi. Hata China baada ya nguvu ya dola kuwa mikononi mwa
Wananchi Rais Mao Tse Tung alisema; “Hamtaki kuangusha nguvu ya Dola? Ndiyo,
tunataka, lakini siyo kwa sasa , hatuwezi kufanya sasa; kwa nini? Kwasababu Ubeberu
bado upo, kwasababu migogoro ya ndani bado ipo, tofauti ndani ya jamii bado ipo. Kazi
yetu kwa sasa ni kuboresha vyombo vya Dola; Jeshi la Ulinzi, Polisi, na Mahakama ili
kuunganisha ulinzi wa Taifa na kuwalinda watu na maslahi yao” Watanzania wangu
msikimbilie kuondoa Dola linaloongozwa na CCM,kwani changamoto zilizopo zinahitaji
pia kuboresha ulinzi na usalama. Wanajeshi waboreshewe maisha yao, ili Ugaidi
umalizwe. Wanajeshi wakazane kuwalinda wasije wakatamani Ikulu kama yaliyonikuta
Mwaka 1964 ambapo nilimkimbia Mpenzi wangu Mariah hadi leo hamjui wengine
husema niliivaa baibui kutorokea Kigamboni, wengine hudai nilijificha Kanisa la St Peter
Oysterbay kila mtu anasema anachojua, msilogwe ndugu zangu Ikulu pagumu.
Waulizeni Sir George Kahama, Job Lusinde Mawaziri wangu Ofisi ya Rais wawaeleze,
aidha,Uchovu alioupata Waziri mwenzao wa Ofisi ya Rais Bwana A.K Hanga
5
unashuhudia Uasi huo huku Kuzimu. Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Ikulu sasa cheo
mnakiita Katibu Mkuu Dkt Amon James Nsekela (1963-1964) anaomba msiguse
machungu ya majonzi dhidi ya Uhaini aliyonayo huku Kuzimu. Aliyempokea na kudumu
kwa muda mrefu Bwana H.K Talawa (1964-1980) na kuteseka pia na vita ya Uganda
anatoa chozi la kuiombea Tanzania Amani. Makatibu Wakuu Viongozi wa wakati huo
Danstun Afred Omari (1962-1964) na Joseph Augustino Namata (1964-1967)
wametandika mikeka huku Kuzimu wakiombolezea Hatma ya Tanzania.
Dhana ya vyama vingi ilenge kujenga umoja; demokrasia ilenge kuwaunganisha kama
ndugu, na Taifa moja. Enzini sera za Kwame Nkrumah wa Ghana na Castro wa Cuba
1969. “Mabadiliko ya utawala yalichukuliwa kuwa siyo kuleta demokrasia, ila
kuwaunganisha Waafrika; mfumo wa utawala wa ukoloni ulizingatia kuengua
demokrasia mpya na ya zamani; na kuweka lengo la mbali la Serikali huru ya Waafrika,
kwa ufupi ulikuwa utawala wa ukoloni wa Waafrika” Hivyo ni vyema kufikiria kuutoa
ukoloni wa kiafrika ndani ya vyama vyenu kuliko kufikiria kuiuwa CCM chama changu
kitakatifu. Ukoloni upo pia kwa CUFists na CHADEmists, kwani nguvu ya vyama vya
upinzani huzuka wakati wa Uchaguzi tu na kujaza ndugu wa kabila moja,dini moja au
Ukanda; hii ni hatari kwa Mustakhbari wa Ikulu endelevu na Taifa kwa ujumla. Hofu ni
kuwa mkichagua UKAWA itachukua muda mrefu kujenga mnyororo wa thamani baina
ya chama kimoja na kingine ndani ya UKAWA, badala ya kuimarisha uchumi na Taifa
endelevu katika nchi yangu; kwani Ikulu itawanogea watu hao. Na hii itahusisha kodi za
Wananchi. Hili ni Angalizo tu sipendi kuhukumu.
CCM yangu; yu heri Edward aliyekengeusha msimamo wake na kukaa kwenye Bwawa
lenye kelele mithiri ya Bwawa lililojaa vyura wajawazito; kuliko Oscar Kambona,
Anangisye, na Wabunge watano tuliowasimamisha Mwaka 1968 kwa kukiuka Imani za
TANU na Sera zake. Mchukulieni Edward kama Kasanga Tumbo kiongozi wa Chama
cha People’s Democratic (PDP) Mbunge aliyewekwa kizuizini kuanzi Januari 1964 hadi
Julai 1966 aliyekuwa mkorofi dhidi ya Sheria ya kuwekwa kizuizini ya tarehe 26
Septemba, 1962; Edward alipinga utaratibu wa ngazi ya mchujo kwa kukengeusha nafsi
yake kisiasa, kuitafuta demokrasia yake Kikatiba, akafuatwa na wengine na sasa ni
mithiri ya Mpiga filimbi wa Hamelini; amejiweka kizuizini ndani ya uwanja wa siasa.
Msishangae ni elimu ya Utamaduni aliyopata Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam na ile ya
Maendeleo yaki-Uchumi aliyoipata Chuo Kikuu cha Barth Marekani, yafaa sasa
alinganishwe na Mwanahisabati na Mkemia Mkufunzi John ili kumpata Mkalia Ikulu
mahala patakatifu.
Siyo ajabu kutofautiana, hata sisi tulipoanzisha Operasheni Vijana tarehe 3 Oktoba
1968 kuzuia nguo fupi zilizoigwa kwa Wazungu, na muziki wa Marekani, alitokea Mkuu
wa Mkoa wa Arusha aliyewahamasisha Wamasai kuacha nguo za Mataifa ya Magharibi
walinde mila, desturi na asili yao wavae nguo zilizowaacha utupu kuliko hata za
Magharibi. Mnamo Agosti, Afisa wa Ubalozi wa China alishindwa kulazimisha uzuiaji wa
picha za Marekani, viatu vya uvuvi, kwavile vilikinzana na Utawala wa China.
Watanzania wangu, maana kwa ajili yenu mmepewa Guru wa kazi, na uweza wa dola la
Ikulu utakuwa begani mwake, naye ataitwa uzao wa ajabu, Rais mwenye nguvu. Ole
wao wapiga kura Wanafiki, maana kilio cha majuto kitakuwa kingi kuliko mafuriko ya
Upendo ya kushangaa Kampeni. Siwakatazi Watanzania wangu, jikusanyeni bila haya
kabla hamjaanza kupiga kura, mtafuteni Rais enyi nyote mlio wanyenyekevu wa
6
Tanzania, itafuteni haki ya Ikulu, kwani miongoni mwa wote waliompenda Edward
hakuna hata mmoja amfarijiye, rafiki zake wote wa kisiasa wamemtenda hila sasa
wamekuwa adui zake anakaa kati ya makafiri wa kisiasa, haoni raha iwayo yote na
wote waliomfuata wamempata katika dhiki yake. Watu wake wote wana tafuta chakula,
yumkini kuwatuhumu kuwa ni Wanafiki.
MUNGU IBARIKI TANZANIA IBARIKI AFRIKA

More Related Content

More from Prof Handley Mpoki Mafwenga

Do mining company able to demonstrate reserves .....
Do mining company able to demonstrate reserves .....Do mining company able to demonstrate reserves .....
Do mining company able to demonstrate reserves .....Prof Handley Mpoki Mafwenga
 
Tax justice and advocacy clinicA Focus on the Revenue Index for Effective Fis...
Tax justice and advocacy clinicA Focus on the Revenue Index for Effective Fis...Tax justice and advocacy clinicA Focus on the Revenue Index for Effective Fis...
Tax justice and advocacy clinicA Focus on the Revenue Index for Effective Fis...Prof Handley Mpoki Mafwenga
 
MASTERS THESIS (ESAMI-MAASTRICHT SCHOOL OF MANAGEMENT -MsM)
MASTERS THESIS (ESAMI-MAASTRICHT SCHOOL OF MANAGEMENT -MsM)MASTERS THESIS (ESAMI-MAASTRICHT SCHOOL OF MANAGEMENT -MsM)
MASTERS THESIS (ESAMI-MAASTRICHT SCHOOL OF MANAGEMENT -MsM)Prof Handley Mpoki Mafwenga
 
The African Interview Questions Between Joyce Mmassy and Prof Handley Mpoki M...
The African Interview Questions Between Joyce Mmassy and Prof Handley Mpoki M...The African Interview Questions Between Joyce Mmassy and Prof Handley Mpoki M...
The African Interview Questions Between Joyce Mmassy and Prof Handley Mpoki M...Prof Handley Mpoki Mafwenga
 
WARAKA WA WATANZANIA KUTOKA AHERA KUHUSU RAIS JAKAYA KIKWETE
WARAKA WA WATANZANIA KUTOKA AHERA KUHUSU RAIS JAKAYA KIKWETEWARAKA WA WATANZANIA KUTOKA AHERA KUHUSU RAIS JAKAYA KIKWETE
WARAKA WA WATANZANIA KUTOKA AHERA KUHUSU RAIS JAKAYA KIKWETEProf Handley Mpoki Mafwenga
 
MHESHIMIWA PINDA HAKUPINDA BALI WANASHERIA WAMECHEUA
MHESHIMIWA PINDA HAKUPINDA BALI WANASHERIA WAMECHEUAMHESHIMIWA PINDA HAKUPINDA BALI WANASHERIA WAMECHEUA
MHESHIMIWA PINDA HAKUPINDA BALI WANASHERIA WAMECHEUAProf Handley Mpoki Mafwenga
 
TEITI -WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA-MWANZA
TEITI -WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA-MWANZATEITI -WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA-MWANZA
TEITI -WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA-MWANZAProf Handley Mpoki Mafwenga
 
WARAKA WA UPENDO KWA JOHN MAGUFURI NA EDWARD LOWASA KUTOKA KWA HAYATI MWAL ...
WARAKA WA UPENDO KWA JOHN MAGUFURI NA EDWARD LOWASA KUTOKA   KWA HAYATI MWAL ...WARAKA WA UPENDO KWA JOHN MAGUFURI NA EDWARD LOWASA KUTOKA   KWA HAYATI MWAL ...
WARAKA WA UPENDO KWA JOHN MAGUFURI NA EDWARD LOWASA KUTOKA KWA HAYATI MWAL ...Prof Handley Mpoki Mafwenga
 
SDGs Tanzania poverty headcount declining as economic growth expands
SDGs Tanzania poverty headcount declining as economic growth expandsSDGs Tanzania poverty headcount declining as economic growth expands
SDGs Tanzania poverty headcount declining as economic growth expandsProf Handley Mpoki Mafwenga
 
LAANA YA RASILIMALI KATIKA SEKTA YA MAFUTA NA GESI ASILIA- Je Tanzania Inawez...
LAANA YA RASILIMALI KATIKA SEKTA YA MAFUTA NA GESI ASILIA- Je Tanzania Inawez...LAANA YA RASILIMALI KATIKA SEKTA YA MAFUTA NA GESI ASILIA- Je Tanzania Inawez...
LAANA YA RASILIMALI KATIKA SEKTA YA MAFUTA NA GESI ASILIA- Je Tanzania Inawez...Prof Handley Mpoki Mafwenga
 
THE OVERSIGHT ROLE OF TANZANIA MINERAL AUDIT AGENCY (TMAA)
THE OVERSIGHT ROLE OF TANZANIA MINERAL AUDIT AGENCY (TMAA)THE OVERSIGHT ROLE OF TANZANIA MINERAL AUDIT AGENCY (TMAA)
THE OVERSIGHT ROLE OF TANZANIA MINERAL AUDIT AGENCY (TMAA)Prof Handley Mpoki Mafwenga
 

More from Prof Handley Mpoki Mafwenga (20)

Do mining company able to demonstrate reserves .....
Do mining company able to demonstrate reserves .....Do mining company able to demonstrate reserves .....
Do mining company able to demonstrate reserves .....
 
East african journal of research
East african journal of researchEast african journal of research
East african journal of research
 
Tax justice and advocacy clinicA Focus on the Revenue Index for Effective Fis...
Tax justice and advocacy clinicA Focus on the Revenue Index for Effective Fis...Tax justice and advocacy clinicA Focus on the Revenue Index for Effective Fis...
Tax justice and advocacy clinicA Focus on the Revenue Index for Effective Fis...
 
MASTERS THESIS (ESAMI-MAASTRICHT SCHOOL OF MANAGEMENT -MsM)
MASTERS THESIS (ESAMI-MAASTRICHT SCHOOL OF MANAGEMENT -MsM)MASTERS THESIS (ESAMI-MAASTRICHT SCHOOL OF MANAGEMENT -MsM)
MASTERS THESIS (ESAMI-MAASTRICHT SCHOOL OF MANAGEMENT -MsM)
 
TAX JUSTICE AND ADVOCACY CLINIC 2
TAX JUSTICE AND ADVOCACY CLINIC  2TAX JUSTICE AND ADVOCACY CLINIC  2
TAX JUSTICE AND ADVOCACY CLINIC 2
 
The African Interview Questions Between Joyce Mmassy and Prof Handley Mpoki M...
The African Interview Questions Between Joyce Mmassy and Prof Handley Mpoki M...The African Interview Questions Between Joyce Mmassy and Prof Handley Mpoki M...
The African Interview Questions Between Joyce Mmassy and Prof Handley Mpoki M...
 
BARUA YA SIRI KWA DR MOHAMED SHEIN TOKA AHELA
BARUA YA SIRI KWA DR MOHAMED SHEIN TOKA AHELABARUA YA SIRI KWA DR MOHAMED SHEIN TOKA AHELA
BARUA YA SIRI KWA DR MOHAMED SHEIN TOKA AHELA
 
WARAKA WA WATANZANIA KUTOKA AHERA KUHUSU RAIS JAKAYA KIKWETE
WARAKA WA WATANZANIA KUTOKA AHERA KUHUSU RAIS JAKAYA KIKWETEWARAKA WA WATANZANIA KUTOKA AHERA KUHUSU RAIS JAKAYA KIKWETE
WARAKA WA WATANZANIA KUTOKA AHERA KUHUSU RAIS JAKAYA KIKWETE
 
MHESHIMIWA PINDA HAKUPINDA BALI WANASHERIA WAMECHEUA
MHESHIMIWA PINDA HAKUPINDA BALI WANASHERIA WAMECHEUAMHESHIMIWA PINDA HAKUPINDA BALI WANASHERIA WAMECHEUA
MHESHIMIWA PINDA HAKUPINDA BALI WANASHERIA WAMECHEUA
 
IKULU SI MAHALA PA KUKIMBILIA HATA KIDOGO
IKULU SI MAHALA PA KUKIMBILIA HATA KIDOGOIKULU SI MAHALA PA KUKIMBILIA HATA KIDOGO
IKULU SI MAHALA PA KUKIMBILIA HATA KIDOGO
 
TEITI -WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA-MWANZA
TEITI -WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA-MWANZATEITI -WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA-MWANZA
TEITI -WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA-MWANZA
 
WARAKA WA UPENDO KWA JOHN MAGUFURI NA EDWARD LOWASA KUTOKA KWA HAYATI MWAL ...
WARAKA WA UPENDO KWA JOHN MAGUFURI NA EDWARD LOWASA KUTOKA   KWA HAYATI MWAL ...WARAKA WA UPENDO KWA JOHN MAGUFURI NA EDWARD LOWASA KUTOKA   KWA HAYATI MWAL ...
WARAKA WA UPENDO KWA JOHN MAGUFURI NA EDWARD LOWASA KUTOKA KWA HAYATI MWAL ...
 
WARAKA WA UPUMBAVU NA ULOFA KATIKA DEMOKRASIA
WARAKA WA UPUMBAVU NA ULOFA KATIKA DEMOKRASIAWARAKA WA UPUMBAVU NA ULOFA KATIKA DEMOKRASIA
WARAKA WA UPUMBAVU NA ULOFA KATIKA DEMOKRASIA
 
SDGs Tanzania poverty headcount declining as economic growth expands
SDGs Tanzania poverty headcount declining as economic growth expandsSDGs Tanzania poverty headcount declining as economic growth expands
SDGs Tanzania poverty headcount declining as economic growth expands
 
LAANA YA RASILIMALI KATIKA SEKTA YA MAFUTA NA GESI ASILIA- Je Tanzania Inawez...
LAANA YA RASILIMALI KATIKA SEKTA YA MAFUTA NA GESI ASILIA- Je Tanzania Inawez...LAANA YA RASILIMALI KATIKA SEKTA YA MAFUTA NA GESI ASILIA- Je Tanzania Inawez...
LAANA YA RASILIMALI KATIKA SEKTA YA MAFUTA NA GESI ASILIA- Je Tanzania Inawez...
 
UFA WA UTEKELEZAJI WA LOCAL CONTENT
UFA WA UTEKELEZAJI WA LOCAL CONTENTUFA WA UTEKELEZAJI WA LOCAL CONTENT
UFA WA UTEKELEZAJI WA LOCAL CONTENT
 
Analysis of the Budget(2)
Analysis of the Budget(2)Analysis of the Budget(2)
Analysis of the Budget(2)
 
EAST AFRICAN JOURNAL OF RESEARCH
EAST AFRICAN JOURNAL OF RESEARCHEAST AFRICAN JOURNAL OF RESEARCH
EAST AFRICAN JOURNAL OF RESEARCH
 
TEKU publication2
TEKU publication2TEKU publication2
TEKU publication2
 
THE OVERSIGHT ROLE OF TANZANIA MINERAL AUDIT AGENCY (TMAA)
THE OVERSIGHT ROLE OF TANZANIA MINERAL AUDIT AGENCY (TMAA)THE OVERSIGHT ROLE OF TANZANIA MINERAL AUDIT AGENCY (TMAA)
THE OVERSIGHT ROLE OF TANZANIA MINERAL AUDIT AGENCY (TMAA)
 

WARAKA WA IKULU TAKATIFU KWA JOHN MAGUFULI, NA EDWARD LOWASA NA HATMA YA TANZANIA

  • 1. 1 WARAKA WA IKULU TAKATIFU KWA JOHN MAGUFULI, NA EDWARD LOWASA NA HATMA YA TANZANIA Na Prof Handley Mpoki Mafwenga Ph.D (finance -COU), MSc (finance -Strathclyde), MBA (Mg.Eco -ESAMI/MsM), LLM (taxation- UDSM), LLB (Tudarco), PGD tax mgt (IFM), AD tax mgt (IFM)] Zamani nikiwa na umri mdogo nilifahamishwa kuwa ukiangalia sana Mwezi utaona Nabii Elia amekalia kiti na amevaa taji, kainama anasikitikia Dunia. Dunia iliyojaa Chuki, Dhiki,Dhambi na Damu ya Uasi wa kiroho. Nikawa naona ni kweli. Katika utu uzima wangu tarehe 7 Septemba, 2015 ghafla naangalia Mwezi naona picha ya John Magufuli, amekalia kiti, kashika Katiba ya Tanzania. Pembeni ya kiti kuna maneno yameandikwa “Ikulu Takatifu” yamezungukwa na maua ya rangi ya kijani na njano; picha ya nembo ya Taifa al-maarufu Adam na Eva na Bendera ya Taifa vimepamba kofia yake. Aidha, kuna imani kuwa, Mawingu hutoa maumbo au picha mbalimbali,mfano ukiliona umbo la samaki ni dalili ya neema kwako; umbo linaloonesha tendo la ndoa ukiliona ni Uchuro hapo kuna kifo au nuksi kubwa; lakini umbo la sura ya mtu ni kiashiria cha mateso na misukosuko ya kutafuta mafanikio bila kuyapata kwa mtu huyo. Naliangalia wingu naona picha ya Edward Lowasa, ina maneno ya Kiingereza No!, No! No! na mengine yakiwa “Ahsante Sana Watanzania, Mungu yu pamoja nami”. Ghafla nazimia namuona Mwalimu Nyerere ameongozana na Wavuta kiko maarufu Sebastian Kinyondo na Kamanda Abdalah Natepe wanavuta kiko zao zinatoa harufu ya udi wanapiga kelele “Tunafukuza harufu ya chuki, damu, ufisadi, na kuilinda Ikulu”. Wananipa Waraka nimpe John Magufuli, Edward Lowasa, na Watanzania usemao; Watanzania wangu, hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa ndiyo wamiliki wa Ikulu kuliko Wagombea wenu? Na kuwa radhi yangu inakaa ndani yenu?. Kama mtu akiiharibu Ikulu kwa kumchagua Mgombea fisadi Mungu atamharibu mtu huyo, kwa maana Ikulu ni mahala patakatifu, na ni miliki ya Taifa lenu. Wagombea wote ni halali, bali si wote watakaoijenga hadhi ya Ikulu kwani John, na Edward wana karama tofauti lakini Tanzania ni ileile. Ikulu ilijengwa na Wajerumani mwaka 1891 na Gavana Chakosi Dikwe na kutumika kama ngome yake, hadhi na siri zake zingali zinakumbukwa huku Kuzimu. Damu za Askari walioiharibu Ikulu wakati wa vita kuu ya kwanza ya dunia inawalilia Wanangu mlio hai. Jasho la Gavana wa kwanza wa kijerumani ndugu Horrace Byatt aliyeboresha Ikulu Mwaka 1919 lingali linalowesha Sanda za Askari hao na kufuta damu zao kila siku. Byatt analia na ananiuliza “Mwalimu Watanzania wanajua kuwa baada ya mimi kuingia madarakani nililazimika kukaa katika makazi ya muda kwenye ofisi zao za wizara ya Afya ili Ikulu iwe Mahala patakatifu?”. Kama mnavyofahamu,
  • 2. 2 Tanganyika ilikuwa chini ya utawala wa Ukoloni wa Waingereza na hapo ngome hiyo (state house) iliitwa Government House na ilijengwa tena mwaka 1922 ambapo gavana wa Kiswahili Sir Unapima Mkali aliyechukua utawala anawalilia Watanzania wasipoteze hadhi ya Ikulu. Ndugu J. H Sinclair - Mtaalam wa majengo wakati wa ukoloni aliyetia nakshi za jengo hilo anawaomba mboreshe Ikulu kwa dhana ya kuchagua Rais safi na alinde Uadilifu. Ikulu maana yake ni Itetemia lenye asili ya Kinyamwezi hasa enzi za mtemi Milambo, Makao Makuu ya ngome ya milambo yenye Uadilifu na hadhi paliitwa kwikulu, ndio neno ikulu likatoholewa. Edward kichwa chake chenye mvi ni taji ya utukufu wa Mashabiki wa siasa wasio na weledi wa uchambuzi, lakini kikionekana katika njia ya haki kitalinda hadhi ya Ikulu na nje ya njia ya haki ni laana ya Watanzania karne na karne zijazo. Ushujaa wa uchapakazi na Uadilifu wa John ni Lulu ya Utulivu na Ushindi wa CCM unaozidi ustawi wa Ngome ya UKAWA yenye karama nyingi zinazojumuisha kuwapoteza Prof Haruna na Padre Mstahafu Wilbroad. Kijana wangu Edward, unafahamu kuwa amdhihakiye Maskini humsuta Muumba wake, unapoongelea Umaskini katika safari ya Ikulu uwe makini, ukifika Ikulu uwe radhi kugawa nusu ya Mali zako kuwapa Maskini; na ujue kuwa changamoto ya Watanzania ni uwezo wa kugawanya rasilimali zao lukuki, Ugawanyaji wa Mapato yao na Uimarishaji wa Uchumi endelevu; dhana ya Umaskini ni Matokeo na siyo chanzo cha Changamoto; aidha, ujue kuwa ajitengaye na CCM hutafuta matakwa yake mwenyewe kwenda Ikulu; je una msingi imara wa muundo wa kichama kuenzi “Utatu wa Elimu” yaani “Elimu, Elimu,Elimu” unaoenzi Azimio langu la Musoma?. Mwanangu Edward nakutakia heri iliyo na nuru kuenzi Elimu maana kumbuka niliwaachia Imani kuwa “Elimu ni Ufunguo wa Maisha”. Kijana wangu John moyo wako umechangamka na ni dawa nzuri ya kukimbilia Ikulu; hekima ipo machoni pako kwani una Ufahamu, isipokuwa uhamasike sana ndani ya Kampeni, hujafika bado Ikulu,usishibe kabla hujala, usioge hujavua nguo; ongeza kasi Ikulu inakukaribia. Tanzania yangu unataka iwe ya Uchumi wa viwanda utakaolinda utajiri wa Mafuta na Gesi ukifungamanishwa na Sekta zingine ili zisije zikafa kwa kukosa nguvu kazi itakayoweza kukimbilia kwenye Mafuta na Gesi, watakakolipwa ujira zaidi na kuacha Sekta zingine kama vile Kilimo. John ndoto zako za kuboresha Ujasilia-Mali ndani ya Uchumi wa viwanda ni wazi utapunguza Umaskini na Kuweka Maendeleo ya Uchumi endelevu; utapunguza gharama za Uzalishaji na kupanua uwezo wa Wananchi kulipa kodi. Lakini nakutakia heri katika jitihada za kufufua viwanda na Ikulu ipo ndani ya mboni zako. Wewe ni Mkemia hapana shaka Viwanda vya mbolea vitapata mtu, uhifadhi wa mazingira utaboreka na ukiwa Mwanahisabati Tanzania itafanya kazi ki-Mahesabu. Ukiwa Ikulu anzisha Mifuko miwili ya Hifadhi ya Mapato ya Mafuta na Gesi; mmoja wa kuimarisha Mapato dhidi ya Mnyumbo wa Uchumi (Stalization Fund), na mwingine wa Uhifadhi wa Mapato kwa Vizazi vijavyo (Saving Fund) ili uchumi wa viwanda uwe endelevu; hiyo iwe sambamba na Uadilifu wa Matumizi ya Mapato.. Nimetambua kuwa kuna vyama vinanipa tabu huku Kuzimu;ACT ni watu wasio na nguvu, lakini hujiwekea Hazina ya kisiasa wakati wa Heri ya Ikulu; NLD ni watu dhaifu lakini hujibanza ndani ya mabawa ya UKAWA huo ni ulaghai wa kisiasa; CHADEMA na CUF hawana Wafalme zao Wilboad na Haruna Ngunyuru waliozama chini ya kivuli
  • 3. 3 kinachoficha demokrasia, lakini vyama hivyo vinakodi Wafalme huku wakienda pamoja vikosi vikosi ndani ya UKAWA; CCM hushika ubora wa Ilani yake wakimiliki Ikulu ya Kivukoni, wakifurahia Upendo kwa nyimbo na lugha zilizojaa Mithali. Vyama hivi huwachanganya Wananchi hawajui mwelekeo na Dira ya Uchaguzi Mkuu. Kijana wangu John, nia yako ya kushughulikia maovu kwa moyo ni yako kama Mwanadamu, jawabu la ulimi wako wenye Upako hutoka kwetu huku Kuzimu na kwa Mungu. Mkabidhi Mungu Sera na Mawazo yako yatathibitika. Ulimi huo ni kama fedha yenye thamani ndani ya soko la ndani na la nje linalopambana na myumbo wa uchumi; fedha itakayofanikisha afya, elimu, maji, umeme na miundombinu laini na migumu, ili Ikulu ithibitike. Matunda yangu na akina Rashid Kawawa, Oscar Kambona, Job Lusinde, Amir Jamar, Nsilo Swai, Tewa Said Tewa, Chief Abdalah Fundikila, Dereck Bryceson, Paul Bomani, Sir Ernest Vasseey, Sir George Kahama, Chief Abdalah Fundikira, Chifu Lukumbuzya, Chief Adam Sapi Mkwawa, Mwami Theresia Ntare na wengine hupita thamani ya dhahabu na vito ndiyo maana Ikulu ililinda Haki. Ukifuata nyendo zangu ni mwanzo wa mwendelezo wa hekima na utakatifu utakaoongeza Ufahamu wako. Mungu amewachukua Mashujaa wangu wote, wachache waliobaki watumieni; Mimi nilipata mateso ya Watanzania na fimbo yangu hadi mkaniita “Musa” na kwavile niliwatoa kwenye bwawa la mateso ya Kikoloni; Mungu aliniongoza katika giza wala si katika nuru nilipokuwa Ikulu; nilichakaa nyama yangu na ngozi yangu; hadi nikafariki mapema kuliko Nelson Mandela kwa kuwapenda Watanzania kubeba mzigo wa Ikulu. Wanangu Watanzania; mmegeuza njia zangu zenye neema, mnararua rarua Sanda yangu; mmenifanya mkiwa huku Butiama kwa ushabiki wa kisiasa, uliokosa tija ya fikra na uchambuzi wa kina. Kumbukeni msiba wangu mlipolia mimi niliililia Ikulu, na Ikulu ilinililia “Baba yangu, Baba yangu wa Taifa Mbona Unaniacha?” nami nikatamka “Unyerere Umekwisha” nikakata roho. Macho yangu yanatoa machozi hayakomi, ningali naililia Ikulu yangu; babu na bibi zenu waliowarithisha Ikulu wanalia, watoto zenu waliowakopesha Ikulu ambao ni samani ya Tanzania wataomboleza kama mtachagua Rais kwa ushabiki wa kisiasa. Wanangu John na Edward, urithi wenu umegeuka kuwa mali ya Wageni na utajiri kuwa mali ya Mafisadi. Watanzania wangu wamekuwa yatima walionyang’anywa urithi wao. Ondoeni pepo la unyonyaji wa rasilimali zetu ili mlinde ushindani wa Wawekezaji wa nje na wa ndani katika Mnyororo wa Thamani wa Uwekezaji; kumbukeni, Kiatu cha Mwanangu Jakaya Kikwete kiliisha sori kulinda hadhi ya Ikulu, aliwatafutia Neema ndani na nje ya nchi; Watanzania walio wengi hamkumsaidia, kazi yenu ikawa kulalama badala ya kufanya kazi, mkitaka akae Msoga aende Ikulu kila siku mithiri ya Mfanyakazi wa kawaida; mkatenganisha Ikulu na Urais kwa kupigwa upofu wa fikra mkilinganisha gharama za Ikulu na za kununua bamia. Lakini mmesahau Yesu Kristo, Mtume Mohammad (S.A.W), Nabii Musa na wengine hawakutulia kuwaletea Waja wa Mola Neema na Ukombozi; yu heri Rais Jakaya Kikwete aliyeenzi Mila na Desturi ya ki- Afrika kuwa Muwindaji (Mfwimi) kwa kuwapa Neema na Ukombozi wa ki-Uchumi. Watanzania wangu, Albino mmewafanya wanyama¸ Binti Kabula Nkalango, Said Abdalah, Nainana Daud,, Rukia Halfan na Fatma Halfan damu zao na viungo vyao vingali vinavuja damu; Wauaji waliohukumiwa kunyogwa; Joseph Lugala,, Masumbuko Madata, Emmanuel Masangwa, Charles Masangwa, Nchenyewe Kisiwa, Sayi Gamaya, Mboje Mawe, Sayi Matizi, na Kazimir Mashauri roho zao zinatuchefua huku Kuzimu;
  • 4. 4 Chozi la Peter Kayanza Pinda halijakauka katika Sanda zetu. Vijana wangu John na Edward mnapokwenda Ikulu zibeni Chemchem ya damu za Albino anzeni alipomalizia Mhe Jakaya. Mama zenu wamekuwa kama wajane mbali ya Mwanangu Jakaya Kikwete kuwajali kwa hali na mali kwa mfano ameteua Wanawake wengi kuwa Majaji, hii ni kuenzi kazi yetu ya tarehe 1 Septemba, 1970 ambapo Tanzania ilikuwa Nchi ya kwanza Afrika Mashariki kuteua Hakimu Mkaazi Mwanamke; tulikuwa na uchache wa Mahakimu Wakazi wakiwa 44 tu kati yao watatu wa-Nigeria, watano wa-Malawi na 36 wa- Tanzania. Jaji Mkuu wa kwanza alikuwa Jaji Said aliyeteuliwa 1971 na Jaji Mkuu wa kwanza wa Mhakama ya Rufaa ya Afrika Mashariki alikuwa Raia wa Tanzania; Ahsante Jakaya Kikwete umetusetiri huku kuzimu akina mama wanakuombea maisha marefu kwani wanaamini majaji wanawake watalinda Utawala wa Sheria mithiri ya binti wa Faraoh aliyelinda Utawala wa Sheria dhidi ya Nabii Musa ndani ya nyumba ya Faraoh baada ya kuokotwa baharini. Nyuso za vikongwe hazipewi heshima huitwa Wachawi utafikiri nyie hamtazeeka, mlidiriki kuchoma nyumba zao zaidi ya 20 wakati mnajua Katiba niliowaachia inazuia Mauwaji,Ukandamizaji na Utesaji ambacho ni kinyume hata cha Sheria ya Makosa ya Jinai na Sheria ya Uchawi ya Mwaka 1928; damu za waliouwawa kwa imani za Uchawi Agripina Thomas, Anamaria Theda, Monica Spron wote wa Kagera, Amana Shawishi wa Mwanza, Lyatoga Venance wa Makongoro Nansio, Cheupe Mwananzyuni wa Rukwa na Frank Mwasha wa Nzega zinaililia Ikulu na Upendo kwa Watanzania; Mabinti zenu wanabakwa na kukatizwa masomo, mabikra ni wa kuhesabu. Watoto wa kiume hulawitiwa kinyume na Kifungu Na 156(1) cha Sheria ya Makosa ya Jinai. Roho zetu zinamuombolezea mtoto wa miaka 13 wa Sumbawanga aliyetelekezwa na mama yake muuza bia bar mjini Mbeya, mtoto aliyefiwa na baba yake akiwa na miaka saba aliyelawitiwa kwa siku tatu na baba wa miaka 51 aliyekuwa akifanya kazi Kampuni ya Majembe Auction Mart Sumbawanga kwavile mtoto aliishi katika mazingira magumu; Aidha, Wakulima na Wafugaji mnauwana mashamba na mifugo imekuwa bora kuliko roho zenu. Enzi zangu moja ya Madhumuni ya Mwongozo wa TANU wa 1971 ilikuwa kulinda maslahi ya Wananchi. Hata China baada ya nguvu ya dola kuwa mikononi mwa Wananchi Rais Mao Tse Tung alisema; “Hamtaki kuangusha nguvu ya Dola? Ndiyo, tunataka, lakini siyo kwa sasa , hatuwezi kufanya sasa; kwa nini? Kwasababu Ubeberu bado upo, kwasababu migogoro ya ndani bado ipo, tofauti ndani ya jamii bado ipo. Kazi yetu kwa sasa ni kuboresha vyombo vya Dola; Jeshi la Ulinzi, Polisi, na Mahakama ili kuunganisha ulinzi wa Taifa na kuwalinda watu na maslahi yao” Watanzania wangu msikimbilie kuondoa Dola linaloongozwa na CCM,kwani changamoto zilizopo zinahitaji pia kuboresha ulinzi na usalama. Wanajeshi waboreshewe maisha yao, ili Ugaidi umalizwe. Wanajeshi wakazane kuwalinda wasije wakatamani Ikulu kama yaliyonikuta Mwaka 1964 ambapo nilimkimbia Mpenzi wangu Mariah hadi leo hamjui wengine husema niliivaa baibui kutorokea Kigamboni, wengine hudai nilijificha Kanisa la St Peter Oysterbay kila mtu anasema anachojua, msilogwe ndugu zangu Ikulu pagumu. Waulizeni Sir George Kahama, Job Lusinde Mawaziri wangu Ofisi ya Rais wawaeleze, aidha,Uchovu alioupata Waziri mwenzao wa Ofisi ya Rais Bwana A.K Hanga
  • 5. 5 unashuhudia Uasi huo huku Kuzimu. Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Ikulu sasa cheo mnakiita Katibu Mkuu Dkt Amon James Nsekela (1963-1964) anaomba msiguse machungu ya majonzi dhidi ya Uhaini aliyonayo huku Kuzimu. Aliyempokea na kudumu kwa muda mrefu Bwana H.K Talawa (1964-1980) na kuteseka pia na vita ya Uganda anatoa chozi la kuiombea Tanzania Amani. Makatibu Wakuu Viongozi wa wakati huo Danstun Afred Omari (1962-1964) na Joseph Augustino Namata (1964-1967) wametandika mikeka huku Kuzimu wakiombolezea Hatma ya Tanzania. Dhana ya vyama vingi ilenge kujenga umoja; demokrasia ilenge kuwaunganisha kama ndugu, na Taifa moja. Enzini sera za Kwame Nkrumah wa Ghana na Castro wa Cuba 1969. “Mabadiliko ya utawala yalichukuliwa kuwa siyo kuleta demokrasia, ila kuwaunganisha Waafrika; mfumo wa utawala wa ukoloni ulizingatia kuengua demokrasia mpya na ya zamani; na kuweka lengo la mbali la Serikali huru ya Waafrika, kwa ufupi ulikuwa utawala wa ukoloni wa Waafrika” Hivyo ni vyema kufikiria kuutoa ukoloni wa kiafrika ndani ya vyama vyenu kuliko kufikiria kuiuwa CCM chama changu kitakatifu. Ukoloni upo pia kwa CUFists na CHADEmists, kwani nguvu ya vyama vya upinzani huzuka wakati wa Uchaguzi tu na kujaza ndugu wa kabila moja,dini moja au Ukanda; hii ni hatari kwa Mustakhbari wa Ikulu endelevu na Taifa kwa ujumla. Hofu ni kuwa mkichagua UKAWA itachukua muda mrefu kujenga mnyororo wa thamani baina ya chama kimoja na kingine ndani ya UKAWA, badala ya kuimarisha uchumi na Taifa endelevu katika nchi yangu; kwani Ikulu itawanogea watu hao. Na hii itahusisha kodi za Wananchi. Hili ni Angalizo tu sipendi kuhukumu. CCM yangu; yu heri Edward aliyekengeusha msimamo wake na kukaa kwenye Bwawa lenye kelele mithiri ya Bwawa lililojaa vyura wajawazito; kuliko Oscar Kambona, Anangisye, na Wabunge watano tuliowasimamisha Mwaka 1968 kwa kukiuka Imani za TANU na Sera zake. Mchukulieni Edward kama Kasanga Tumbo kiongozi wa Chama cha People’s Democratic (PDP) Mbunge aliyewekwa kizuizini kuanzi Januari 1964 hadi Julai 1966 aliyekuwa mkorofi dhidi ya Sheria ya kuwekwa kizuizini ya tarehe 26 Septemba, 1962; Edward alipinga utaratibu wa ngazi ya mchujo kwa kukengeusha nafsi yake kisiasa, kuitafuta demokrasia yake Kikatiba, akafuatwa na wengine na sasa ni mithiri ya Mpiga filimbi wa Hamelini; amejiweka kizuizini ndani ya uwanja wa siasa. Msishangae ni elimu ya Utamaduni aliyopata Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam na ile ya Maendeleo yaki-Uchumi aliyoipata Chuo Kikuu cha Barth Marekani, yafaa sasa alinganishwe na Mwanahisabati na Mkemia Mkufunzi John ili kumpata Mkalia Ikulu mahala patakatifu. Siyo ajabu kutofautiana, hata sisi tulipoanzisha Operasheni Vijana tarehe 3 Oktoba 1968 kuzuia nguo fupi zilizoigwa kwa Wazungu, na muziki wa Marekani, alitokea Mkuu wa Mkoa wa Arusha aliyewahamasisha Wamasai kuacha nguo za Mataifa ya Magharibi walinde mila, desturi na asili yao wavae nguo zilizowaacha utupu kuliko hata za Magharibi. Mnamo Agosti, Afisa wa Ubalozi wa China alishindwa kulazimisha uzuiaji wa picha za Marekani, viatu vya uvuvi, kwavile vilikinzana na Utawala wa China. Watanzania wangu, maana kwa ajili yenu mmepewa Guru wa kazi, na uweza wa dola la Ikulu utakuwa begani mwake, naye ataitwa uzao wa ajabu, Rais mwenye nguvu. Ole wao wapiga kura Wanafiki, maana kilio cha majuto kitakuwa kingi kuliko mafuriko ya Upendo ya kushangaa Kampeni. Siwakatazi Watanzania wangu, jikusanyeni bila haya kabla hamjaanza kupiga kura, mtafuteni Rais enyi nyote mlio wanyenyekevu wa
  • 6. 6 Tanzania, itafuteni haki ya Ikulu, kwani miongoni mwa wote waliompenda Edward hakuna hata mmoja amfarijiye, rafiki zake wote wa kisiasa wamemtenda hila sasa wamekuwa adui zake anakaa kati ya makafiri wa kisiasa, haoni raha iwayo yote na wote waliomfuata wamempata katika dhiki yake. Watu wake wote wana tafuta chakula, yumkini kuwatuhumu kuwa ni Wanafiki. MUNGU IBARIKI TANZANIA IBARIKI AFRIKA