1. Singachini TTC 2012
JEDWALI LA KUTAHINI
Kabla mwalimu hajaanza kutunga maswali anapaswa kutayarisha jedwali la kutahini. Jedwali la kutahini ni utaratibu
unaonyesha maada za kupima na idadi ya maswali kwa kila maada. Jedwali hili huonyesha malengo yanatarajiwa
kufikiwa pamoja na idadi ya maswali kwa kila maada na/au idadi ya maswali kwa kila ngazi inayopimwa. Jedwali
hupangwa kwa safu. Safu ya kwanza upande wa kushoto huwekwa maudhui kwa kuorodhesha maada(kuu/ndogo)
zinazopimwa. Safu inayofuata kulia huwekwa malengo ya kupimwa,inayofuata nyanja inayopimwa na ngazi zake.
Watahini wengi hutumia mgawanyo wa Bloom (1956) kuainisha stadi hizo. Hata hivyo hufungwi na
utaratibu huu ikiwa somo lako haliwezi kupimwa kikamilifu kwa mgawanyo huo.unaweza kuweka
utaritibu mwingine kama utaona unafaa zaidi.
Idadi ya maswali huonyeshwa katika mkato wa chumba cha maudhui kuelekea kulia na kile cha safu ya ngazi ya stadi
zinazopimwa.
Jumla ya maswali kwa kila maada huandikwa upande wa kulia na Jumla ya maswali kwa kila ngazi ya Nyanja
inayopimwa (mara nyingi utambuzi) huandikwa kwenye mstari wa chini ya jedwali.
Mfano wa Jedwali la Kutahini
STADI ZA KUPIMWA JUMLA
MALENGO ASILIMIA
MAADA ZA KWA
YA Nganzi Ngazi Ngazi Ngazi Ngazi KWA KILA
KUPIMWA …… KILA
KUPIMWA 1 2 3 4 5 MADA
MADA
Mada A
Mada B
Mada C
…
JUMLAYA
MASWALI
KWA KILA
NGAZI
ASILIMIA
KWA KILA
NGAZI
Prepered by Adam Chaula
College Tutor II Page 1
2. Singachini TTC 2012
UTAYARISHAJI WA JEDWALI LA KUTAHINI
Mambo ya kufanya wakati wakuandaa jedwali la kutahini.
1. Chukua muhtasari wa somo na maandalio ya somo.
2. Chunguza katika maandalio ya somo maada ambazo zimekishwa fundishwa.
3. Chagua mada ambazo unaona ni muhimu zitungiwe jaribio/ mitihani kisha orodhesha mada hizo.
4. Chunguza kwa makini katika muhtasari na maandalio ya somo malengo mahsusi ya mada zinazotungiwa
maswali.
Orodhesha malengo hayo kisha amua:
i. aina ya maswali yatakayotumika katika upimaji.
ii. idadi ya maswali yote katika mitihani.
iii. muda wa kufanya jaribio hutegemea na wingi wa mada na hali ya malengo yenyewe
5. Chora jedwali la kutahini.
6. Jaza jedwali la kutahini kwa kufuata hatua hizi.
i. orodhesha mada zote za kutungiwa maswali.
ii. orodhesha malengo mahususi katika safu inayofuata
iii. Amua ngazi zipi za nyanja ipi za kupimwa zipewe umuhimu wa kupewa maswali mengi na zipi zipewe
maswali machache.
UMUHIMU WA JEDWALI A KUTAHINI
1. Linahakikisha kuwa maudhui yote yanayotakiwa kutahiniwa yanatahiniwa.
2. Linahakikisha kuwa kiwango cha kuelewa maarifa , kumudu stadi za utendaji na kubadilika kwa mwelekeo
wa watahiniwa kinatahiniwa
3. Linahahakikisha uwiano wa idadi ya maswali katika kila eneo na kila kipengele cha nyanja kinapimwa .
Prepered by Adam Chaula
College Tutor II Page 2
3. Singachini TTC 2012
Mfano wa Jedwali la kutahini wa somo la Maarifa ya Jamii
JEDWALI LA KUTAHINI KWA SOMO LA MAARIFA YA JAMII DARASA LA TANO
MUHULA WA II, 2012
NYANJA YA MWELEKEO
Kuwa tayari ASILIMIA
Kuwianisha
Kutathmini
Msimamo
MADA ZA MALENGO YA JUMLA KWA
maswala
kuitikia
KWA KILA
KUPIMWA KUPIMWA KILA MADA
MADA
Mahusiano
ya jamii za 1 2 3 15%
Tanzania
Mila na
1 1 1 3 15%
desturi
Kufanya
1 1 1 3 15%
kazi
Kusoma
1 2 3 15%
ramani
Muundo wa
serikali ya 2 1 3 15%
kijiji
Ushiriki wa
2 3 5 15%
jamii
IDADI YA MASWALI KWA
5 6 2 4 3 20 15%
KILA NGAZI
ASILMIA KWA KILA NGAZI 25% 30% 10% 20% 15% 100% 100%
Prepered by Adam Chaula
College Tutor II Page 3