Ce diaporama a bien été signalé.
Nous utilisons votre profil LinkedIn et vos données d’activité pour vous proposer des publicités personnalisées et pertinentes. Vous pouvez changer vos préférences de publicités à tout moment.

Survey questionaire instrument kiswahili

373 vues

Publié le

vvvcccccc

 • Here's How YOU Can Stake Out Your Personal Claim In Our EIGHT MILLION DOLLAR GOLDMINE...  https://bit.ly/2Ruzr8s
     Répondre 
  Voulez-vous vraiment ?  Oui  Non
  Votre message apparaîtra ici
 • Soyez le premier à aimer ceci

Survey questionaire instrument kiswahili

 1. 1. 1 CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM IDARA YA SAYANSI YA SIASA NA UTAWALA DODOSO KUHUSU UWEZESHWAJI WA JAMII KUSHINIKIZA UTEKELEZAJI WA UWAJIBIKAJI KATIKA FEDHA ZA HUDUMA ZA AFYA KATIKA HALIMASHAURI YA WILAYA YA KASULU Mpendwa Mshiriki , ChuoKikuu cha Dar es Salaam kupitia wafanyakazi na wanafunzi wake hufanya tafiti zinazolenga kuchangia katika uelewa na utatuzi wa matatizo muhimu yanayoathiri Jamii za Tanzania na Nyinginezo. Mimi Respicius Shumbusho Damian ni Mwanafunzi mtaaluma katika Shahada ya Uzamivu ambapo nafanya utafiti kuhusu Uwajibikaji katika Fedha za Huduma za Afya Kupitia Njia Mbalimbali katika Ngazi ya Jamii, hasa jamii za vijijini. Kama mmoja wa waliochaguliwa kushiriki, naomba mchango wako katika utafiti huu kupitia maswali machache ambayo yatachukua takribani dakika 45 hadi 60. Nakuhakikishia kuwa majibu utakayoyatoa ni kwa ajili ya uchambuzi wa kitaaluma tu na hayatatumika vinginevyo. Pia nakuhakikishia kuwa hautatajwa kwa mtu yeyote yule kama chanzo cha habari au majibu youyote utakayotupatia. Ushiriki wako ni wa hiari na bure. Jisikie huru kujiondoa katika utafiti huu au kutojibu swali ambalo hautapendezwa nalo muda wowote. SEHEMU A. UTAMBULISHO WA SAMPULI NA DEMOGRAPHIA ZA MSINGI 1. Jina la Kata 1) Bugaga 2) Rungwe Mpya 3) Nyakitonto 4) Titye 2. Jina la Kijiji 1) Bugaga 2) Nkundutsi 3) Rungwe 4) Kaguruka 5) Nyakitonto 6) Mugombe 7) Titye 8) Lalambe 3. Jinsi 1) Mume 2) Mke 4. Hali ya ndoa 1) Nimeoa/Nimeolewa (hadi sasa) 2) Sijaolewa (kabisa) 3) Nimeachika/Nimetalakiwa 4) Mjane/mgane 5. Umri wa mshiriki (miaka)
 2. 2. 2 1) 18-35 (kijana) 2) 36-50 (mtu mzima umri wa kati) 3) 51-59 (mtu mzima wa makamo) 4) 60-70 (mzee wa makamo) 5) 71 au zaidi (mzee -kikongwe) 6. Ngazi ya juu ya elimu ya darasani uliyoipata 1) Sijamaliza elimu ya msingi 2) Elimu ya msingi 3) Elimu ya sekondari 4) Shahada ya chuo kikuu 5) Elimu ya juu nyingine (siyo shahada) 7. Hali ya ajira ya sasa ya mshiriki 1) Ameajiliwa 2) Hana ajira 3) Amestaafu katika ajira 8. Kazi kuu ya mshiriki inayomwingizia kipato 1) Mkulima (kilimo cha mazao/kufuga wanyama) 2) Ajira katika sekta rasmi 3) Kujiajili katika biashara ndogondogo 4) Mama/baba wa nyumbani anategemea kipato cha mwenza wake 5) Mwanafunzi 6) Mengineyo (baini)__________________ 9. Mahitaji maalumu ya kiafya 1) Mlemavu (ulemavu wa aina yoyote) 2) Mama mjamzito 3) Mzee zaidi ya miaka 60 4) Mengineyo (elezea)_________________ 5) Hana mahitaji maalumu ya kiafya 10. Makadirio ya kipato cha wastani cha kaya kulinganisha na kaya nyingine katika kijiji 1) Chini sana ya wastani 2) Chini ya wastani 3) Wastani 4) Juu ya wastani 5) Juu sana ya wastani 11. Aina ya kaya ukizingatia uongozi wa kaya na muundo wa familia 1) Kaya yenye familia kamilifu (enye baba, mama, watoto) 2) Kaya ya familia yenye baba na watoto 3) Kaya ya familia yenye mama na watoto 4) Kaya isiyo na muundo wa kifamilia mf. Geto, Masikani, n.k
 3. 3. 3 5) Nyinginezo (eleza)_________________________________ 12. Makadirio kutoka sehemu inapopatikana huduma ya afya iliyo Karibu mfano Zahanati au kituo cha afya 1) Karibu zaidi ya kilomita moja (dakika chache kuliko 12) 2) Kati ya kilomita 1 na 2.9(dakika 12-35.59) 3) Kati ya kilomita 3 na 4.9 (dakika 36-59:59) 4) B Kati ya kilomita 5 na 6.9 (dakika 60-83.59) 5) Kilomita 7 au zaidi (dakika 84 au zaidi) SEHEMU B: JITIHADA ZA KUAMSHA JAMII KUDAI UWAJIBIKAJI WA FEDHA 13. Je umewahi kuhudhuria kampeni au mafunzo yoyote yanayohamasisha wanajamii kuhoji juu ya uwajibikaji wa watoa huduma za afya? 1) Ndiyo [Kama ndiyo jibu swali la 14] 2) Hapana [Kama hapana ruka swali la 14] 14. Kama jibu lako kwenye swali la 13 ni “ndiyo”, nani waliendesha kampeni au mafunzo hayo? [zungushia yote yanayohusika] 1) Redio ya ngazi ya Jamii (taja)___________________________________________ 2) Asasi za kiraia katika Jamii yetu (taja)_____________________________________ 3) Makundi ya kufaana kijamii (taja)________________________________________ 4) Maafisa wa serikali za Mitaa (taja wadhifa)________________________________ 5) Viongozi waliochaguliwa na wananchi (taja wadhifa)________________________ 6) Asasi zisizo za kiserikali kutoka sehemu nyingine (taja)______________________ 15. Je, umewahi kuhudhuria kongamano/warsha yoyote yenye lengo la kuwashirikisha wanajamii katika kuweka vipaumbele, Mipango ya fedha, na ufuatiliaji wa matumizi ya fedha zilizopo kwa ajili ya afya ya Jamii? 1) Ndiyo. Nimewahi kusikia na kuhudhuria 2) Ndiyo. Nimewahi kusikia lakini sijahudhuria 3) Hapana. Sikuwahi kusikia wala kuhudhuria [Kama chagui lako katika swali la 15 ni 2 au 3 ruka swali la 16 na kujibu swali la 17] 16. Kama umewahi kusikia na kushiriki katika warsha au kongamano lililotajwa katika swali la 15. Ni kwa kiwango gani makomanano/warsha za namna hiyo zimekuwa zikiitishwa mara kwa mara katika eneo unaloishi? 1) Mara nyingi sana 2) Mara nyingi 3) Wastani 4) Mara chache 5) Mara chache sana 17. Ni kwa kiasi gani unaweza kukubali kuwa Asasi Za Kiraia (AZAKI) zinatoa mchango wake katika kuhamasisha wananchi kushiriki katika kufuatilia fedha kawa ajili ya utoaji wa huduma za afya katika eneo unaloishi? 1) Nakubaliana kabisa
 4. 4. 4 2) Nakubaliana 3) Sina chaguo 4) Sikubaliani 5) Sikubaliani kabisa 18. Ni kwa kiasi gani unaweza kukubali kuwa Makundi ya Kufaana Kijamii yanayopatikana katika eneo unaloishi yanapewa kipaumbele kushiriki katika kuhamasisha wananchi kushiriki katika kufuatilia fedha kawa ajili ya utoaji wa huduma za afya katika eneo unaloishi? 1) Nakubaliana kabisa 2) Nakubaliana 3) Sina chaguo 4) Sikubaliani 5) Sikubaliani kabisa 19. 18. Ni kwa kiasi gani unaweza kukubali kuwa Asasi Za Kiraia zinatoa mchango wa kutosha katika kuwapatia wananchi taarifa muhimu wanazohitaji ili kuweza kushinikiza uwajibikaji katika utoaji wa huduma za afya? 1) Nakubaliana kabisa 2) Nakubaliana 3) Sina chaguo 4) Sikubaliani 5) Sikubaliani kabisa 20. Ni kiasi gani unaweza kusema kuwa taarifa za matumizi ya fedha za afya zinawekwa wazi kwa wananchi mara kwa mara katika eneo unaloishi? 1) Mara nyingi sana 2) Mara nyingi 3) Wastani 4) Mara chache 5) Mara chache sana 21. Iwapo taarifa za fedha zinawekwa wazi katika eneo unaloishi, ni njia gani zinatumika kuwafikishia wananchi taarifa hizo? 1) Taarifa zilizochapishwa na kuwekwa kwenye mbao za matangazo 2) Taarifa zilizochapishwa husomwa na kuelezewa kwenye mikutano 3) Nakala za taarifa zilizochapishwa husambazwa kwa wananchi 4) Maafisa Watendaji wa Vijiji hutoa maelezo ya mdomo(bila maandishi) 5) Mengineyo(eleza)________________________________________ SEHEMU C: VIASHIRIA VYA KUTATHMINI UWEZESHWAJI WA WANAJAMII B1 (a) Viashiria vifuatavyo vitatuwezesha kufanya tathmini na kuelewa uwezo wako kama mwananchi kuchangia katika utekelezaji wa uwajibikaji katika matumizi ya fedha kwa ajili ya huduma za afya. Kwa kila kiashiria, baini kiwango cha uwezo wako kati ya 1 na 5 ambapo viwango vya tathmini vinaweza kutafsiriwa ifuatavyo: 1=uwezo mdogo sana, 2=uwezo mdogo, 3=wastani, 4=uwezo mkubwa, 5=uwezo mkubwa sana
 5. 5. 5 1 2 3 4 5 22 Kuwa na taarifa za kutosha kuhusu vyanzo vya fedha zinazotumika kugharamia huduma za afya kwa wanajamii eneo unaloishi 23 Kujisikia utayari wa kuchangia fedha kwa ajili ya utoaji wa huduma za afya kwa wanajamii eneo unaloishi. 24 Kujisikia kuwa na uhakika wa kutosho kuweza kupata taarifa zenye kukuwezesha kuhoji juu ya mgawanyo na matumizi ya fedha za huduma za afya kwa Jamii. 25 Kujisikia kuwa ni haki yako kupata habari juu ya jinsi gani fedha zilizopo kwa ajili ya huduma za afya zitatumika. 26 Kujisikia kuwa na uwezo wa kushawishi katika maamuzi ya uwekaji vipaumbele katika matumizi ya fedha kwa ajili ya huduma za afya. 27 Kuwa na uwezo wa kusoma na kuelewa taarifa za fedha zinazohusu mgawanyo na matumizi ya fedha za afya. 28 Kuwa na ujuzi unaohusiana na Mipango ya fedha na uchambuzi wa matumizi bora ya fedha 29 Kuelewa/kuwa na habari juu ya uwepo wa Kamati ya Zahanati 30 Kujua wawakirishi wa wananchi/jamii katika kamati ya zahanati 31 Kujisikia kuwa wawakilishi katika kamati za Zahanati wanawakilisha vipaumbele vyangu kuhusu huduma za afya. 32 Kujisikia kuwa viongozi waliochaguliwa wana uwezo wa kutosha kushawishi watendaji wa afya kutenda kadri ya mahitaji (ya kiafya)ya Jamii 33 Kujua kazi na wajibu wa kamati za zahanati 34 Kijisikia kuwa unaweza kwenda ofisi ya Afisa Mtendaji wa Kijiji na kumtaka akupatie taarifa ya matumizi ya fedha za afya. 35 Kujisikia kuwa unaweza kuwahitaji watoa huduma za afya kutoa huduma bora 36 Kujisikia kuwa ni wajibu wako kuhakikisha fedha zilizopo/zilizotengwa kawa ajili ya afya hazitumiki vibaya. 37 Kuamini kuwa viongozi katika ngazi ya Jamii/kijiji wana uwezo wa kutosha kufuatilia na kushinikiza matumizi bora ya fedha kwa niaba ya wananchi? 38 Kujisikia kuwa maafisa wa serikali wanaohusika na utawala wa fedha za huduma za afya wanasimamia maslahi ya wananchi 39 Kuwa na uhakika kuwa serikali hutenga na kutoa fedha kwa ajili ya huduma za afya kwa Jamii unayoishi 40 Kuamini kuwa fedha zinazotengwa kwa ajili ya huduma za afya zinasimamiwa ipasavyo. SEHEMU D. TATHMINI YA JUMLA (YA USHAWISHI, KUJIAMINI, NA USIKIVU) 41. Ni kwa kiwango gani unaweza kukubali kuwa maslahi yako kama mwananchi yanapewa kipaumbele katika kupangilia matumizi ya raslimali zilizopo kwa ajili ya kugharamia huduma za afya?
 6. 6. 6 1) Nakubaliana kabisa 2) Nakubaliana 3) Sina chaguo 4) Sikubaliani 5) Sikubaliani kabisa 42. Ni kwa kiwango gani unaweza kukubali kuwa watendaji wa serikali wenye dhamana ya kupitisha Mipango ya matumizi ya fedha katika huduma za afya wanazingatia mahitaji/vipaumbele vya kiafya vya wananchi katika eneo unaloishi? 1) Nakubaliana kabisa 2) Nakubaliana 3) Sina chaguo 4) Sikubaliani 5) Sikubaliani kabisa 43. Kiujumla, ni jinsi gani unaweza kutathmini uwezo wako mwenyewe wa kushawishi katika maamuzi yanayohusu jinsi gani fedha zilizotengwa kwa ajili ya kutoa huduma za afya Jamii unayoishi zigawanywe/zitumike? 1) Mdogo sana 2) Mdogo 3) Wastani 4) Mkubwa 5) Mkubwa sana 44. Kiujumla, ni jinsi gani unaweza kutathmini utendaji wa Jumla wa kamati za vituo vya afya/Zahanati katika kudhibiliti uwekaji vipaumbele na matumizi bora ya fedha ili kutoa huduma bora za afya? 1) Wa chini sana 2) Wa chini 3) Wa wastani 4) Wa juu 5) Wa juu sana E. MASWALI MENGINE 45. Je, kaya yenu ina watu ambao wanapata huduma za afya kupitia njia ya Tiba kwa Kadi (yaani kuchangia fedha kwenye mfuko wa afya ya Jamii na kupata huduma kwa kadi? 1) Ndiyo 2) Hapana ASANTE KWA USHIRIKIANO WAKO

×