1. ELIMU YA WATU WAZIMA
• Katika mada hii tunajifunza:
1. Maana ya Elimu ya Watu Wazima.
2. Sifa na mahitaji ya wanafunzi watu wazima.
3. Umuhimu wa EWW.
4. Mikakati ya utekelezaji wa EWW Tanzania.
5. Muundo wa uendeshaji wa EWW Tanzania.
6. KCM &KCK.
2. MAANA YA ELIMU YA WATU
WAZIMA
• Ili kuelewa vizuri maana ya EWW
inabidi kuelewa mambo yafuatayo:
• Maana ya elimu
• Mtu mzima ni nani?
• Mwanafunzi mtu mzima ni nani?
• Mapana ya elimu ya watu wazima.
• Nani walengwa wa EWW.
3. MAANA YA ELIMU
• Ni tendo la kupata na kutumia misingi ya ujuzi,
maarifa na muelekeo inayomuwezesha mtu
kuishi ipasavyo katika jamii.
• Ni jumla ya mambo yote ya kuhusuyo ujuzi,
stadi,maarifa na mwelekeo katika jamii.
• Elimu ni chombo cha ukombozi na ni chombo
hutusaidia katika kutatua matatizo mbalimbali
ili kuweza kupambambana na mazingira yetu
vizuri.
4. MTU MZIMA NI NANI?
• Ni yule mwenye umri wa miaka
kumi na nane (18) na kuendelea
kutokana na sifa zifuatazo:
I. Kuweza kupiga kura
II. Kuoa/ kuolewa
III. Kugombea uongozi kuhukumiwa
kifungo cha ndani (magereza).
5. MWANAFUNZI MTU MZIMA NI NANI?
• Ni mtu anayejitambua, anaejitegemea na aliye
na ujuzi na uzoefu mwingi wa mambo
mbalimbali kutokana na kuishi kwake muda
mrefu kwenye majukumu ya kifamilia na
kijamii ambayo anayakubali na kuyakabili.
• Pia yuko tayari kujifunza kwa kwa bidii ili
aweze kuyakabili vilivyo mazingira yake .
6. MAPANA YA ELIMU YA WATU
WAZIMA
• EWW ni eneo pana sana ambalo ni pamoja ya
kujifunza jambo lolote lenye shabaha ya
kumwendeleza mwanadamu aweze
kuyamudu mazingira yake.
• Mfano :
• Elimu ya jadi,kisomo cha kujiendeleza,
masomo ya jioni, elimu kwa redio/ tv,
masomo kwa njia ya posta n.k.
7. WALENGWA WA EWW
• Kwa ujumla ni watu wazima ambao hupata
mafunzo ya elimu kwa mfumo usio wa kishule.
• Ki umri ni tangu anaestahili kuanza shule ya
msingi na amevuka umri huo.
• Ki elimu ni tangu asiejua kusoma na kuandika
hadi aliye na elimu ya juu (chuo kikuu).
• Kishughuri ni watuwote. Wakulima, wafanya
biashara na wengineo.
8. MAANA YA EWW
• Kwa mtazamo wa kimataifa, EWW ni elimu
yoyote inayotolewa kwa mtu aliye na umri wa
miaka 18 na kuendelea.
• Nchini Tanzania maana hii inashindwa kuwa
sahihi kutokana na utoaji wake, matakwa ya
elimu hii katika jamii na mfumo mzima wa
elimu wa nchi hii ambao ni 7:4:2:3+
9. Mwendelezo………..
• Hata hivyo maana ya EWW kwa kigezo cha umri
ina utata kwani kuna wale wanaopitia mfumo wa
eww wakiwa na umri chini ya miaka 18.
• Hivyo kushiriki katika darasa la EWW
kunabadilika kutokana na mahitaji ya jamii.
• Mwanafalsafa J.K. Nyerere alitoa maana ya EWW
kuwa ni “ Harakati za binadamu kujifunza kitu
chochote kile ambacho kitamsaidia kuelewa
mazingira anayoishi na jinsi atakavyoyakabiri.
10. Mwendelezo…………..
• Mawazo ya wataalamu wengine juu ya EWW.
• Tunapozungumzia juu ya EWW tunaweza
tukamainisha aina yoyote ya mpango wa
elimu wapatayo watu baada ya masomo yao
ya shule.
• Tunaweza tukamaanisha aina ya Elimu
itolewayo kwa watu waliokisha komaa tayari.
• (E.M. Hutchson-President Europian Bureau of Adul Education)
11. Mwendelezo……
• ….. EWW ni nguvu ambayo ikitumiwa vema
huleta mabadiliko ya fikra katika jamii ya watu
kwa muda mfupi iwezekanavyo.
• (Roy Prosser- Adult education Developing countries).
12. SIFA NA MAHITAJI YA MWANAFUNZI MTU
MZIMA
1. Uzoefu wa mambo mbalimbali katika jamii
kivitendo na kinadharia.
2. Kukomaa kwa akili.
3. Kukomaa kimaumbile.
4. Haiba nzuri na kujiheshimu.
5. Kuwa na busara na ushari mzuri kwa wengine.
6. Kuwa na majukumu mbalimbali ya kifamilia na
ya kijamii.
13. Mwendelezo………
7.Kujitambua na kujiamini binafsi.
8. Uwezo wa kujiongoza mwenyewe na
kujitegemea.
9. Kuheshimiwa na kutambuliwa na watu
wengine.
10. Kutegemewa na familia, ndugu na jamaa
zake pamoja na jamii nzima.
14. UMUHIMU WA EWW
• Humuwezesha mtu kutoka kwenye hali duni
ya maisha ambayo watanzania wamekuwa
wakiishi kwa karne nyingi zilizopita.
• Humwezesha mtu kujifunza jinsi ya kuinua hali
ya maisha yake kwa kufanya kazi kwa bidii na
kuzalisha mali zaidi, kuboresha afya yake na
na kutengeneza thamani zake,kutengeneza
zana zake na kufanya kazi mbalimbali.
15. Mwendelezo……..
• Kumfanya mtanzania aelewe sera ya chama
tawala na ya vyama vingine vya siasa katika
harakati za kuleta maendeleo ya watanzania.
• Kutoa elimu ya uongozi kwa viongozi wa
Tanzania katika ngazi zote.
• Kufuta ujinga wa kutojua kusoma, kuandika na
kuhesabu.
• Husaidia kutoa ujuzi wa kazi mbalimbali na
mwamko wa siasa; n.k.
16. Mwendelezo……..
• EWW husaidia kutoa ujuzi na maarifa ya aina
mbalimbali kwa mfano kilimo, biashara, ufundi
mbalimbali n.k.
• Kutoa elimu kwa shule za msingi na sekondari
zenye mtaamo wa kumtayarisha mlengwa aweze
kuishi vizuri vijijini na mjini kwa kuzingatia siasa
na sheria za nchi yetu.
• Kusaidia kusawazisha pengo la elimu miongoni
mwa watanzania.
18. MIKAKATI YA UTEKELEZAJI WA EWW TANZANIA
• Tangu 1961 EWW imechukuliwa kuwa ni kati
ya mambo ya kwanza kwa umuhimu katika
maendeleo ya taifa letu.
• Mpango wa kwanza wa maendeleo ya miaka
mitano (1964-1969) uliweka mkazo kwenye
EWW.
• mpango wa pili wa maendeleo wa miaka
mitano(1969-1974) serikali ilichukua jukumu
jipya ktk kuongoza na kutekeleza EWW.
19. Mwendelezo…….
• Kutangaza mwaka 1970 kuwa mwaka wa EWW
kuliongeza nguvu zaidi.
• Tangu kipindi hiko hadi sasa kumekuwa na
mikakati ifuatayo:
• Kuundwa kwa idara ya EWW.
• Kuanzishwa kwa elimu ya wafanyakazi.
• Kuanzisha kwa mabaraza ya wafanyakazi.
• Kuteuliwa kwa wizara sita katika kampeni ya
kufuta ujinga.(Mafia, Ukerewe,kilimanjaro,Pare, masasi na dar es salaam).
20. Mwendelezo…….
• Kuanzishwa kwa kampeni mbalimbali nchini
mfano:
• Mtu ni afya(1970).
• Uchaguzi ni wako (1970).
• Wakati wa furaha (1971).
• Chakula ni uhai (1975).
• Kufuta ujinga(1971-75). N.k.
• Kuanzishwa kwa chama cha elimu ya watu
wazima Tanzania (CHEWATA).
21. Mwendelezo…….
• Kuanzishwa kwa taasisi ya EWW (1975).
• UPE kwa ajili ya kufuta ujinga.
• Kuanzishwa kwa vyuo vya maendeleo ya wananchi 1975.
• Mpango wa maendeleo wa 1964-1969 ulikuwa na lengo la
kuwaonesha Watanzania kuwa EWW ni haki ya kila mtu.
• Agizo la WM(1973):Kuazishwa kwa Idara ya Wafanyakazi
– baada ya muda iliitwa Idara ya Elimu na ushirikishwaji wa
Wafanyakazi 2.5.1974
• Kuanzishwa kwa vituo vya EWW katika kila mkoa.
• Kuanzishwa kwa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania(OUT),n.k
22. MUUNDO WA UENDESHAJI WA EWW, TZ
Afisa Elimu Vielelezo EWW Afisa Elimu Maarifa ya
Nyumbani
23. Mwendelezo………
• Baada ya kutangazwa kuwa mwaka 1970 ni
mwaka wa EWW nchini Tanzania;kulianza
mipangilio mbalimbali ili kurahisisha
utekelezaji