SlideShare une entreprise Scribd logo
1  sur  2
20/07/2017
RISALA YA CHAWAKAMA-KENYA KWA CHAKITA
Kwa Mstahiki Mwenyekiti wa CHAKITA, kamati kuu CHAKITA, wageni waheshimiwa mlio
safiri kutoka janibu mbalimbali za Jumuiya yetu adhimu ya Afrika Mashariki, wapenzi na
wakereketwa wa Kiswahili hamjambo.
Natua fursa hii kwanza kutoa shukran zangu za dhati kwa CHAKITA kwa kufaulisha msururu
wa makongamano nchini. Kongole kwa kwa juhudi za dhati za kukuza na kuendeleza Kiswahili.
Asateni kwa kukiunga chama cha wanafunzi CHAWAKAMA-KENYA mkono. Kamati kuu ya
chama hicho inatoa shukran za dhati kupitia risala hii kwa wahadhiri wetu ambao wameendelea
kuwa walezi wa vyama vyetu vyuoni. Tunashukuru sana
Ninafuraha kubwa kutoa risala hii mbele yenu ikiwa ni mara ya kwanza kabisa kwa historia ya
CHAWAKAMA-KENYA kuanzishwa mwaka wa 2004. Asante kwa kutupa fursa hii adimu.
Kwa minajili ya kumbukumbu zetu, CHAWAKAMA ni chama cha wanafunzi wa Kiswahili
Afrika Mashariki. Chama hichi hujumuisha wanafunzi wote wanaotaalimia kozi mbalimbali za
Kiswahili vyuonI kuanzia kwa Elimu, Sanaa na Uanahabari. Nchini Kenya tumefaulu kuvileta
vyuo zaidi ya 26 pamoja na kuwashirikisha wanafunzi wanaofanya kozi za Kiswahili katika
makongamano yetu ya kila mwaka. Bado uhamasisho unaendelea vyuoni kwa lengo la kuwaleta
wakereketwa wanafunzi wengi zaidi pamoja.
CHAWAKAMA Kenya kimegawanywa katika makanda mawili: kanda ya mashariki na kanda
ya magharibi. Kila kanda huanda kongamano na kuvishirikisha vyuo vinavyopatikana katika
kanda husika, hata hivyo, ruwaza ya mahudhurio imebadilika hivi kwamba huwezi kurejelea
kongamano la kanda fulani kwa wanfunzi wa makanda yote wanashiriki vyema. Kimsingi kanda
ya magharibi huandaa kongamano lake kila mwezi wa kumi na moja na kanda la mshariki
huanda kongamano la kila mwezi wa Januari. Mwezi wa Machi huwa ni wa kongamano la
kimataifa na ambalo hudumu kwa siku tatu. Licha ya makongamano ya ndani ya nchi,
CHAWAKAMA Kenya hushiriki kwenye makongamano ya kimataifa. Tumehudhuria
makongamano ya kimataifa kwanzia mwaka 2010:
2010 - Mkutano ulikuwa chuo kikuu cha Dodoma- Tanzania
2011 - Chuo kikuu cha Bishop Stewart Mbarara- Uganda
2012 - Chuo kikuu cha Burundi-Bujumbura.
2013 - Taasisi ya Elimu Rwanda-Kigali
2014 - Chuo Kikuu cha Laikipia-Kenya
2015 - Chuo Kikuu cha Kyambogo, Kampala-Uganda
2016 - Chuo Kikuu cha SUZA,Zanzibar
2017-Chuo Kikuu cha Burundi, Burundi.
Mwaka jana tumekuwa na wajumbe 49 kisiwa Zanzibar. Mwaka huu mahamasiho yamepamba
moto vyuoni tayari kwa kongamano la Bujumbura-Burundi.
Tumepata ufanisi mkubwa chini ya ulezi wa Dkt. Sheila Wandera. Sasa chama kimesajiliwa
rasmi na msajili wa vyama na tuna cheti rasmi ya serikali. CHAWAKAMA Kenya ndicho chama
pekee miongoni mwa vyama vya wanafunzi ambacho huhifadhi makala yote yaliyowasilishwa
kwenye makongamano. Kwa sasa karibu tunasimama dede. Tuna miswada mine ya jarida letu
“Mwanga Afrika Mashariki”
Ndugu waheshimiwa licha ya ufanisi huu mkubwa, majarida yenyewe yameendelea kubaki tu
miswaada na kuozea kwenye rafu za wahariri wa CHAWAKAMA. Binafsi nilikuwa mwasisi wa
wazo la kuandaa jarida kwa lengo la kuhifadhi kazi mbalimbali za wanafunzi na majarida haya
kutumiwa kama nyezo yaakufunzia wale hawakujua kuandaa karatasi za kiakademia.
Wastahiki mtatu poteza sie kizazi tunaopenda Kiswahili katika karne hii msipotuwaun/i.
Tumehaadiwa na wengi tu wenye majina na vyeo kuwa tutasaidiwa kuchapisha. Ahadi hizo zote
huishia ukumbini. Baada ya makongamano mambo hutulia kama maji ya mtunguni. Hivyo leo
tunaomba mwenyekiti CHAKAMA kwa ushirikiano na mkurugenzi wa TATAKI kutusaidia kwa
uhariri wa kina na machapisho ya majrida yetu.
Pia tunawatuma kwa wapendwa wanafunzi kuwashauri kujiunga na CHAWAKAMA Kenya na
kuhudhuria mikutano yetu mikuu ya kila mwaka. Ni ombi letu pia kuwa CHAKITA kichukue
hatua za kufuatilia shughuli za CHAKITA, mawasilisho ili kuhakikisha ubora na utaalamu
unadumishwa. Fauka ya hayo pia CHAKITA kiwe msingi imara kuendeleza Kiswahili kupitia
wanachama vyuoni. Pia tunaomba CHAKITA na chakima kutuombea ufadhili kutoka ofisi za
mabalozi wananchi mbalimbali na zaidi ya yote tume ya Kiswahili katika Jumuiya ya Afrika
Mashariki kwa kuwa wanafunzi wengi wameendelea kujifadhili kuhudhuria makongamanano
mbalimabli.
Asante sana kwa kunisikiliza. Mungu awabariki sana
Ofisa katika kamati ya Nidhamu CHAWAKAMA-KENYA
Eric Juma Omondi

Contenu connexe

En vedette

How to Prepare For a Successful Job Search for 2024
How to Prepare For a Successful Job Search for 2024How to Prepare For a Successful Job Search for 2024
How to Prepare For a Successful Job Search for 2024Albert Qian
 
Social Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie Insights
Social Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie InsightsSocial Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie Insights
Social Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie InsightsKurio // The Social Media Age(ncy)
 
Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024
Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024
Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024Search Engine Journal
 
5 Public speaking tips from TED - Visualized summary
5 Public speaking tips from TED - Visualized summary5 Public speaking tips from TED - Visualized summary
5 Public speaking tips from TED - Visualized summarySpeakerHub
 
ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd
ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd
ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd Clark Boyd
 
Getting into the tech field. what next
Getting into the tech field. what next Getting into the tech field. what next
Getting into the tech field. what next Tessa Mero
 
Google's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search Intent
Google's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search IntentGoogle's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search Intent
Google's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search IntentLily Ray
 
Time Management & Productivity - Best Practices
Time Management & Productivity -  Best PracticesTime Management & Productivity -  Best Practices
Time Management & Productivity - Best PracticesVit Horky
 
The six step guide to practical project management
The six step guide to practical project managementThe six step guide to practical project management
The six step guide to practical project managementMindGenius
 
Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...
Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...
Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...RachelPearson36
 
Unlocking the Power of ChatGPT and AI in Testing - A Real-World Look, present...
Unlocking the Power of ChatGPT and AI in Testing - A Real-World Look, present...Unlocking the Power of ChatGPT and AI in Testing - A Real-World Look, present...
Unlocking the Power of ChatGPT and AI in Testing - A Real-World Look, present...Applitools
 
12 Ways to Increase Your Influence at Work
12 Ways to Increase Your Influence at Work12 Ways to Increase Your Influence at Work
12 Ways to Increase Your Influence at WorkGetSmarter
 
Ride the Storm: Navigating Through Unstable Periods / Katerina Rudko (Belka G...
Ride the Storm: Navigating Through Unstable Periods / Katerina Rudko (Belka G...Ride the Storm: Navigating Through Unstable Periods / Katerina Rudko (Belka G...
Ride the Storm: Navigating Through Unstable Periods / Katerina Rudko (Belka G...DevGAMM Conference
 
Barbie - Brand Strategy Presentation
Barbie - Brand Strategy PresentationBarbie - Brand Strategy Presentation
Barbie - Brand Strategy PresentationErica Santiago
 
Good Stuff Happens in 1:1 Meetings: Why you need them and how to do them well
Good Stuff Happens in 1:1 Meetings: Why you need them and how to do them wellGood Stuff Happens in 1:1 Meetings: Why you need them and how to do them well
Good Stuff Happens in 1:1 Meetings: Why you need them and how to do them wellSaba Software
 
Introduction to C Programming Language
Introduction to C Programming LanguageIntroduction to C Programming Language
Introduction to C Programming LanguageSimplilearn
 
En vedette (20)

How to Prepare For a Successful Job Search for 2024
How to Prepare For a Successful Job Search for 2024How to Prepare For a Successful Job Search for 2024
How to Prepare For a Successful Job Search for 2024
 
Social Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie Insights
Social Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie InsightsSocial Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie Insights
Social Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie Insights
 
Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024
Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024
Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024
 
5 Public speaking tips from TED - Visualized summary
5 Public speaking tips from TED - Visualized summary5 Public speaking tips from TED - Visualized summary
5 Public speaking tips from TED - Visualized summary
 
ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd
ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd
ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd
 
Getting into the tech field. what next
Getting into the tech field. what next Getting into the tech field. what next
Getting into the tech field. what next
 
Google's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search Intent
Google's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search IntentGoogle's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search Intent
Google's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search Intent
 
How to have difficult conversations
How to have difficult conversations How to have difficult conversations
How to have difficult conversations
 
Introduction to Data Science
Introduction to Data ScienceIntroduction to Data Science
Introduction to Data Science
 
Time Management & Productivity - Best Practices
Time Management & Productivity -  Best PracticesTime Management & Productivity -  Best Practices
Time Management & Productivity - Best Practices
 
The six step guide to practical project management
The six step guide to practical project managementThe six step guide to practical project management
The six step guide to practical project management
 
Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...
Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...
Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...
 
Unlocking the Power of ChatGPT and AI in Testing - A Real-World Look, present...
Unlocking the Power of ChatGPT and AI in Testing - A Real-World Look, present...Unlocking the Power of ChatGPT and AI in Testing - A Real-World Look, present...
Unlocking the Power of ChatGPT and AI in Testing - A Real-World Look, present...
 
12 Ways to Increase Your Influence at Work
12 Ways to Increase Your Influence at Work12 Ways to Increase Your Influence at Work
12 Ways to Increase Your Influence at Work
 
ChatGPT webinar slides
ChatGPT webinar slidesChatGPT webinar slides
ChatGPT webinar slides
 
More than Just Lines on a Map: Best Practices for U.S Bike Routes
More than Just Lines on a Map: Best Practices for U.S Bike RoutesMore than Just Lines on a Map: Best Practices for U.S Bike Routes
More than Just Lines on a Map: Best Practices for U.S Bike Routes
 
Ride the Storm: Navigating Through Unstable Periods / Katerina Rudko (Belka G...
Ride the Storm: Navigating Through Unstable Periods / Katerina Rudko (Belka G...Ride the Storm: Navigating Through Unstable Periods / Katerina Rudko (Belka G...
Ride the Storm: Navigating Through Unstable Periods / Katerina Rudko (Belka G...
 
Barbie - Brand Strategy Presentation
Barbie - Brand Strategy PresentationBarbie - Brand Strategy Presentation
Barbie - Brand Strategy Presentation
 
Good Stuff Happens in 1:1 Meetings: Why you need them and how to do them well
Good Stuff Happens in 1:1 Meetings: Why you need them and how to do them wellGood Stuff Happens in 1:1 Meetings: Why you need them and how to do them well
Good Stuff Happens in 1:1 Meetings: Why you need them and how to do them well
 
Introduction to C Programming Language
Introduction to C Programming LanguageIntroduction to C Programming Language
Introduction to C Programming Language
 
Risala ya chawakama

  • 1. 20/07/2017 RISALA YA CHAWAKAMA-KENYA KWA CHAKITA Kwa Mstahiki Mwenyekiti wa CHAKITA, kamati kuu CHAKITA, wageni waheshimiwa mlio safiri kutoka janibu mbalimbali za Jumuiya yetu adhimu ya Afrika Mashariki, wapenzi na wakereketwa wa Kiswahili hamjambo. Natua fursa hii kwanza kutoa shukran zangu za dhati kwa CHAKITA kwa kufaulisha msururu wa makongamano nchini. Kongole kwa kwa juhudi za dhati za kukuza na kuendeleza Kiswahili. Asateni kwa kukiunga chama cha wanafunzi CHAWAKAMA-KENYA mkono. Kamati kuu ya chama hicho inatoa shukran za dhati kupitia risala hii kwa wahadhiri wetu ambao wameendelea kuwa walezi wa vyama vyetu vyuoni. Tunashukuru sana Ninafuraha kubwa kutoa risala hii mbele yenu ikiwa ni mara ya kwanza kabisa kwa historia ya CHAWAKAMA-KENYA kuanzishwa mwaka wa 2004. Asante kwa kutupa fursa hii adimu. Kwa minajili ya kumbukumbu zetu, CHAWAKAMA ni chama cha wanafunzi wa Kiswahili Afrika Mashariki. Chama hichi hujumuisha wanafunzi wote wanaotaalimia kozi mbalimbali za Kiswahili vyuonI kuanzia kwa Elimu, Sanaa na Uanahabari. Nchini Kenya tumefaulu kuvileta vyuo zaidi ya 26 pamoja na kuwashirikisha wanafunzi wanaofanya kozi za Kiswahili katika makongamano yetu ya kila mwaka. Bado uhamasisho unaendelea vyuoni kwa lengo la kuwaleta wakereketwa wanafunzi wengi zaidi pamoja. CHAWAKAMA Kenya kimegawanywa katika makanda mawili: kanda ya mashariki na kanda ya magharibi. Kila kanda huanda kongamano na kuvishirikisha vyuo vinavyopatikana katika kanda husika, hata hivyo, ruwaza ya mahudhurio imebadilika hivi kwamba huwezi kurejelea kongamano la kanda fulani kwa wanfunzi wa makanda yote wanashiriki vyema. Kimsingi kanda ya magharibi huandaa kongamano lake kila mwezi wa kumi na moja na kanda la mshariki huanda kongamano la kila mwezi wa Januari. Mwezi wa Machi huwa ni wa kongamano la kimataifa na ambalo hudumu kwa siku tatu. Licha ya makongamano ya ndani ya nchi, CHAWAKAMA Kenya hushiriki kwenye makongamano ya kimataifa. Tumehudhuria makongamano ya kimataifa kwanzia mwaka 2010: 2010 - Mkutano ulikuwa chuo kikuu cha Dodoma- Tanzania 2011 - Chuo kikuu cha Bishop Stewart Mbarara- Uganda 2012 - Chuo kikuu cha Burundi-Bujumbura. 2013 - Taasisi ya Elimu Rwanda-Kigali 2014 - Chuo Kikuu cha Laikipia-Kenya
  • 2. 2015 - Chuo Kikuu cha Kyambogo, Kampala-Uganda 2016 - Chuo Kikuu cha SUZA,Zanzibar 2017-Chuo Kikuu cha Burundi, Burundi. Mwaka jana tumekuwa na wajumbe 49 kisiwa Zanzibar. Mwaka huu mahamasiho yamepamba moto vyuoni tayari kwa kongamano la Bujumbura-Burundi. Tumepata ufanisi mkubwa chini ya ulezi wa Dkt. Sheila Wandera. Sasa chama kimesajiliwa rasmi na msajili wa vyama na tuna cheti rasmi ya serikali. CHAWAKAMA Kenya ndicho chama pekee miongoni mwa vyama vya wanafunzi ambacho huhifadhi makala yote yaliyowasilishwa kwenye makongamano. Kwa sasa karibu tunasimama dede. Tuna miswada mine ya jarida letu “Mwanga Afrika Mashariki” Ndugu waheshimiwa licha ya ufanisi huu mkubwa, majarida yenyewe yameendelea kubaki tu miswaada na kuozea kwenye rafu za wahariri wa CHAWAKAMA. Binafsi nilikuwa mwasisi wa wazo la kuandaa jarida kwa lengo la kuhifadhi kazi mbalimbali za wanafunzi na majarida haya kutumiwa kama nyezo yaakufunzia wale hawakujua kuandaa karatasi za kiakademia. Wastahiki mtatu poteza sie kizazi tunaopenda Kiswahili katika karne hii msipotuwaun/i. Tumehaadiwa na wengi tu wenye majina na vyeo kuwa tutasaidiwa kuchapisha. Ahadi hizo zote huishia ukumbini. Baada ya makongamano mambo hutulia kama maji ya mtunguni. Hivyo leo tunaomba mwenyekiti CHAKAMA kwa ushirikiano na mkurugenzi wa TATAKI kutusaidia kwa uhariri wa kina na machapisho ya majrida yetu. Pia tunawatuma kwa wapendwa wanafunzi kuwashauri kujiunga na CHAWAKAMA Kenya na kuhudhuria mikutano yetu mikuu ya kila mwaka. Ni ombi letu pia kuwa CHAKITA kichukue hatua za kufuatilia shughuli za CHAKITA, mawasilisho ili kuhakikisha ubora na utaalamu unadumishwa. Fauka ya hayo pia CHAKITA kiwe msingi imara kuendeleza Kiswahili kupitia wanachama vyuoni. Pia tunaomba CHAKITA na chakima kutuombea ufadhili kutoka ofisi za mabalozi wananchi mbalimbali na zaidi ya yote tume ya Kiswahili katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kuwa wanafunzi wengi wameendelea kujifadhili kuhudhuria makongamanano mbalimabli. Asante sana kwa kunisikiliza. Mungu awabariki sana Ofisa katika kamati ya Nidhamu CHAWAKAMA-KENYA Eric Juma Omondi