Practices and drivers of antibiotic use in Kenyan smallholder dairy farms
Kufikia maendeleo Jumuishi ya tasnia ya maziwa Tanzania
1. Kufikia Maendeleo Jumuishi ya Tasnia ya Maziwa Tanzania
Mkutano wa Kitaifa wa Wadau wa Maendeleo ya Tasnia ya Maziwa
Tarehe 22 Februari 2013 katika hoteli ya Blue Pearl, Dar es Salaam
Imetayarishwa na
Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB)
Chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA)
International Livestock and Research Institute (ILRI)
Heifer Project International (HPI)
SNV - The Netherlands Development Organisation
Land O’ Lakes, Inc
Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi (MLDF)
Lengo la Mkutano ni
kujadili Madhumuni ya Jukwaa la Wadau wa
Maendeleo ya Tasnia ya Maziwa
1. Kukuza mwelekeo wa umoja katika uwekezaji wa umma na
binafsi katika tasnia ya maziwa
2. Kukuza Weledi na njia bora za kuendeleza tasnia ya maziwa
3. Kuwa na Jukwaa kwa ajili ya kupeana habari na
kubadilishana ujuzi ikiwa ni pamoja na :
• Jukwaa kuwa chombo cha kitaifa cha kuwakutanisha
wadau wa maziwa mara kwa mara na kutoa ubunifu wa
utaratibu wa kutatua matatizo sugu katika tasnia ya
maziwa hivyo kujenga ushirikiano katika kutatua
matatizo
• Kuwezesha uanzishwaji wa majukwaa ya maziwa ya
ubunifzu ya kikanda
Tunategemea kusikia nini katika mkutano huu
• Kutakuwa na mada itakayoelezea muundo, kazi, na uwanachama wa Jukwaa hilo iliyotayarishwa na kikosi
kazi kilichoteuliwa wakati wa mkutano wa nane (8) wa Baraza la Wadau wa Maziwa wakati wa Wiki ya
Maziwa iliyofanyika mjini Moshi Mei 2012.
• Mitazamo ya vyama vya wadau juu ya ajenda ya baadaye ya Jukwaa la wadau wa maziwa (DDF) iwe nini
• Warsha kuweza kuzalisha orodha ya awali ya changamoto na matatizo muhimu katika tasnia ya maziwa
ambayo yanahitaji kushughulikiwa
Tunategemea nini kutoka kwenu….
• Ushiriki wenu katika kuainisha na kutengeneza orodha ya awali ya matatizo na changamoto zinayoikabili
tasnia ya maziwa
• Wewe utashiriki vipi katika kutatua matatizo na changamoto yaliyoainishwa