SlideShare une entreprise Scribd logo
1  sur  9
Télécharger pour lire hors ligne
12/8/2013

MBUKE TIMES

TAFAKARI ZETU

www.mbuke.blogspot.com | www.facebook.com/mbuketimes
Tafakari zetu

2013

Tafakari yetu leo:
Inawezekana Suluhu ipo karibu sana ila tatizo wewe unafikiria upande mmoja tuu!
--Jifunze toka ktk hadithi hii fupi: Mmama mmoja aliyekuwa akioga alitoka mkuku
bafuni baada ya kusikia sauti ya picha ya X, toka chumbani kwa watoto wake. Kufika
kweli watoto wake wenye umri wa miaka 6-10 walikuwa wakiangalia picha. Yeye
kwa haraka akatoa khanga aliyokuwa amejifunga na kuifunika TV, yeye akabaki
mtupu huku akiwakemea watoto. Mara baba naye aliyekuwa anajiandaa kuvaa
chumbani akakurupuka akiwa kajifunga taulo tuu, kufika chumbani kwa watoto
akaanza kumkaripia mkewe kuwa si vizuri kukaa mtupu mbele ya watoto hivyo
akavua taulo na kumfunika mkewe, huku akimlaumu.
--Ndio hivyo kuna nyakati waweza kujikuta unadhani suluhu ni moja tuu, kumbe
ukifikiria zaidi waweza pata njia nyingi ya kupata suluhu ya magumu unayokumbana
nayo. Fikiri kabla ya kufanya maamuzi hususani maamuzi mazito kama
Mapenzi,Fedha,ajira, malezi ya watoto n.k
Tafakari Yetu leo:
Umekwisha sikia mara nyingi watu wakisema " Aaah mtu ukishamfahamu, hakupi
shida".
-- Leo nakutaka utumie msemo huo kwako mwenyewe yaani jiambie "
Nikishajifahamu sintojipa shida".
Kisha anza juhudi za kujifahamu kweli kweli, fanya bidii kukumbuka kwa kila wakati
na tukio husika jinsi kujifahamu kwako kunavyoweza kusaidia au kutokukusaidia
katika kutimiza majukumu yako ya msingi. Mfano:
Unajifahamu vipi kuhusu matumizi ya fedha ?-basi ukiwa na mshahara au pato lolote
kuwa makini
Unajifahamu vipi kuhusu mapenzi -wivu na kujali? -basi kuwa makini
Unajifahamu vipi kuhusu kujifunza mambo mapya ? -Badilisha hali isiyokusaidia
kama vile kutokupenda kusoma.
--Usijipe shida, JIFAHAMU, chukua hatua kurekebisha yasiyokusaidia.
Tafakari yetu leo:
Ukiwa darasani haileti maana kunyoosha mkono ili kujibu swali wakati haujui jibu.
Mwalimu akikuchagua ukasimama na kusema haujui jibu, ni kujidhalilisha.
Iweje leo unatafuta kazi wakati hauna ujuzi ulichosomea zaidi ya cheti tuu?
Iweje unatafuta schorlaship wakati matokeo yao shule iliyopita ni ya kuunga unga,
hata lugha mama ya elimu-english inakupiga chenga.
Epuka mawazo ya kila kitu utaweza kwa kuunga unga. Jiwezeshe kuwa bora ktk
mambo ya msingi.
Tafakari zetu

2013

Tafakari yetu leo:
Wanasema wanawake TISA hawawezi kushirikiana kubeba ujauzito ili kujifungua
mtoto ndani ya MWEZI MMOJA.
---Sio kila ushirikiano unaoutafuta utakuletea mafanikio. Ushirikiano mwingine (team
work) waweza rudisha nyuma maendeleo au isilete matarajio kabisa. Jifunze wakati
fulani kufanya mambo wewe mwenyewe kwa ufanisi zaidi.
Tafakari yetu:
Kila kukicha dunia inabadilika, fursa na hatari zinaongezeka. Ni mbaya kama uwezo
wako wa ufahamu haubadiliki. Mfano ajira haitegemei tena aina gani ya elimu
uliyonayo bali uwezo na utayari wako wa kufanya kazi fulani. Lugha za kigeni na
kompyuta hazihitajiki tena kuwa tuu kwenye cheti chako bali ni nyenzo haswa za
'kukutoa'.
--Huu si muda wa kungoja kutafutwa, bali wewe mwenyewe chukua hatua ya
kujiweka mbele ili uonekane.
--Kila mtu sasa ni mzalishaji au mteja wako mtarajiwa, angalia unavyoonekana
mbele ya wazalishaji wenzako na wateja wako watarajiwa. Muonekano wako na
ufahamu wako utatumika kukuhukumu ktk kukupatia 'dili' na kufungua njia ya
mafanikio yako.
Tafakari yetu ni kuwa:
Hauhitaji kujirusha toka ghorofa ya 20 kujua kama unaweza kufa kwa kufanya hivyo.
---Hivyo usiwe mgumu kuchukua tahadhali kuhusu ukimwi kwakuwa bado
haujakukuta.
Tafakari yetu leo:
Fanya likupasalo kwa nguvu zako zote na maarifa yako yote bila kuhofu ni kwa
kiwango gani ufanyacho kitaonekana BORA, kwani ubora wa jambo hautegemei tuu
ufanyacho- mara nyingi hutegemea tafsiri za watu, muda uliopo, vitu vingine
vilivyopo, taarifa ambazo watu wanazo, na zaidi sana uwepo wa watu wengine
wafanyao kitu kama chako.
--Inasikitisha watu hawajadili ubora wa kitu au mtu kwa kuangalia kitu au mtu
mwenyewe bali mambo mengi kama hayo ndio maana leo simu za mche wa sabuni
si mali tena, Messi ni bora zaidi ya Ronaldo, na hatari hata kwa wapenzi
wanafananishwa na waliopita au watu tuu wengine huko mitaani. Hata MBUKE
TIMES ni mbaya, ukilinganisha na blog nyingine uifikiriayo ni bora!
Tafakari zetu

2013

Tafakari yetu leo ni:
Ukiota ndoto nzuri unatamani iwe kweli, na hautamani iwe kweli -usingizini, bali
unatamani iwe kweli katika maisha yako halisi-wakati umekwisha amka.
---Ndivyo ilivyo, kama unawaza na kutamani mambo mazuri katika maisha yako acha kuendelea kulala kijuhudi, kimawazo, kimbinu, na kimazingira. Mambo
yanabadilika kila siku, amka sasa uanze kutekeleza unayotamani.
Maneno matupu, mipango mitupu bila utekelezaji ni sawa na kuendelea kulala ukiota
ndoto nzuri ambayo haikusaidii chochote huko usingizini hata kama ndoto hiyo
inasema umekwa bilionea namba 1 dunia nzima.
Tafakari yetu leo ni :
Usikubali Teknolojia ichukue nafasi ya ubinadamu wako kwa kujiaminisha kuwa
unaweza kuishi maisha ya namna mbili-moja ya hapa mtandaoni (FB) kwa lugha
mbovu, ukajipa majina yasiyo yako, na kuandika "utakavyo" na nyingine eti wewe ni
mtu mstaarabu na mwenye muelekeo wa maisha , mtu wa kutegemewa.
--Labda tuu uwe na mkakati madhubuti katika kufanya hivyo, ila kujipa maisha
yasiyo yako hapa mtandaoni kuna madhara mengi kwako kuliko faida zake.
Unachoandika(kusema) ndicho kilichomo akilini mwako, na kilichomo akilini ndicho
kinachokufanya uwe hivyo ulivyo, na ndivyo watu watakavyokuelewa.
Tafakari yetu leo:
Kigumu zaidi katika kujiletea mabadiliko sio ugumu wa kutenda unayopaswa kufanya
ili kuleta mabadiliko bali ni Ugumu wa wewe kukubali kuwa mabadiliko
yanawezekana, na kwamba wewe unaweza kubadilika.
--Busara inaanza na kuweza kuji-amrisha kufanya tofauti na
uliyokwishazoea,kuishinda hofu,na kufuta mengi uliyokwisha jifunza. JISHINDE
WEWE MWENYEWE.
Tafakari Yetu leo:
Ukiacha familia gani umezaliwa, au nchi gani umezaliwa na uwepo wa bahati hapa
na pale, chunguza kwa makini utagundua kushindwa kwako katika mambo mengi ni
kwa sababu yako wewe mwenyewe !
--Hata hivyo una haki ya kushinda, unaweza kubadilika sasa na kuishi maisha ya
ushindi. Fikiria kwa mapana, anza hata ikibidi kidogo kidogo kujiletea mabadiliko.
Tafakari zetu

2013

Tafakari yetu leo:
MAMBO YASIPOENDA SAWA LEO,KUMBUKA IPO KESHO PIA!
Kuna utofauti mkubwa kati ya KUTUMAINI na KUTARAJIA kufanyika kwa jambo
fulani.
1. Kutumaini kunakuruhusu kufikiria njia mbadala na kuwa na subira bali kutarajia ni
kuwa na mtazamo wa aina moja na kutojiandaa au kutokuwa tayari kuchagua au
kutafakari njia mbadala.
2.Kutumaini mara nyingi hakuleti maumivu makali kulinganisha na KUTARAJIA
hususani pale mambo yanapoenda sivyo ndivyo. Mfano UNATUMAINI mtu atafanya
kitu fulani ukimpatia kitu fulani, asipofanya sio shida sana, kuliko UKITARAJIA kabisa
kuwa atafanya halafu asifanye,utabaki UNAHUZUNIKA.
Tafakari yetu leo:
Ingawa bahati ipo na pia tunafanya maombi lakini kumbuka maandalizi na juhudi ya
kile unachotamani ni ya msingi, na pengine maandalizi na juhudi zako zinaweza
kuwa SUMAKU ya BAHATI.
--Chukulia mfano una kiingereza cha "kuokoteza" halafu unapata ufadhili wa kusoma
UINGEREZA, ila kwanza unatakiwa ufanye interview ya ana kwa ana masaa mawili
na timu ya wafadhili wako ! Utajikuta hivi hivi unaiacha bahati !
Tafakari yetu leo:
Kumbuka ili kufanikiwa sio lazima ufanye kitu KIKUBWA au kwa USTADI mkubwa
sana bali la msingi ni kufanya toka moyoni na kwa juhudi ya kiwango chako cha juu
kabisa.
--Biashara nyingi kubwa hazikuanza zikiwa kubwa, kuna makosa mengi mengi
yalifanyika kabla ndege ya kwanza haijaanza kuruka hewani, kuna hasara nyingi
katika ugunduzi mbalimbali kama baruti (niliandika hapa MBUKE TIMES) hata hivyo
uduni wa mwanzo wa hayo ni historia tuu, hakuna anayetilia maanani.
-Au basi embu jikumbushe SIMU za mkononi zilipotoka,enzi za "mche wa
sabuni"mpaka Iphone.
--Anza sasa kujishughulisha kwa ajili ya ndoto yako.
Tafakari yetu:
Mambo yafuatayo yanaweza onekana kama msaada katika kuleta furaha kwetu, hata
hivyo kwa baadhi imekuwa kinyume,yanaongeza GHARAMA ya kuwa na FURAHA:
1. Utajiri
2. Marafiki wenye mafanikio
3. Mpenzi /Mke Mzuri
4. Ajira
5.Watoto
--Zaidi ya kutafuta vitu tunavyodhani vitatupatia furaha tutumie muda pia kuboresha
Tafakari zetu

2013

UFAHAMU wetu, tujitambue na tufanye akili zetu ziwe huru. Na zaidi sana TUMCHE
MUNGU.
Tafakari yetu leo:
Watoto wanapoanza kujifunza kusoma huanza na A E I O U. Hata hesabu huanzia
kuhesabu 1, 2, n.k. Hata hivyo leo hii wewe uliyeanza na A E I O U, unachat
FB,kama vile sio yule ambaye A E I O U zilikuwa zinamsumbua !
--Mambo mazuri na makubwa huanza kidogo kidogo
-Tukumbushane kaugonjwa ka kushindwa kuchukua hatua ya kuanza jambo la
msingi! Hatua shuleni, makazini, katika mahusiano, biashara , n.k.
--Kama hamasa umeshapata sana, kama masomo na mbinu hizo ulizonazo unaweza
anza nazo kufanya jambo la msingi. Hata hivyo wengi tunasubiri mpaka tuwe na
uwezo wa kufanya "jambo kubwa".
Usingoje "uwezo mkubwa", anza kidogo kidogo, uzoefu utakaoupata na makosa
utakayofanya yatakusaidia kujiweka vema hapo baadae.
Tafakari yetu leo ni:
"Usiogope kihivyo kuwa dunia itaisha leo hii Jumatano, kumbuka kuna nchi nyingine
Jumatano yako kwao bado ni Jumanne, au ndio Alhamis yao "
--- La msingi katika tafakari hii ni kuwa ingawa woga ni muhimu wakati fulani, ila
angalia pia na vitu vya kuogopa! Vitu vingine unaogopa ni kwakuwa tuu hauna
taarifa sahihi !
Tafakari yetu leo:
Kirahisi rahisi huwa tunawaambia wengine tunawapenda na tupo tayari kufanya
lolote kwa ajili yao.
Tugeuze kibao sasa…
Inaweza kuonekana kama jambo rahisi rahisi hivi, ila embu fikiria WEWE
UNAJIPENDA KWELI KWELI .
1. Je ni kwa kiwango gani unajali afya yako: Ili uweze kuwepo kwa miaka mingi zaidi
2. Je ni kwa kiwango gani una juhudi ya kutafuta mambo ya kuboresha ufahamu
wako, kupata busara zaidi ili uongeze nafasi za kuwa na furaha ( Kwa kuwa FURAHA
kwa kiwango kikubwa ni vile tunavyochukulia mambo –kifikra zetu na fikra zetu
zinaboreshwa au kudhoofishwa na kiwango cha ufahamu, uzoefu na makuzi yetu)
3. Je ni kwa kiwango gani una juhudi katika kufanya bidii ya kazi ya kukupatia kipato
, au una zuga zuga tuu ugange njaa
4. Je ni kwa kiwango gani unafanya mazingira uliyopo yawe masafi na salama ili
wewe ubaki kuwa salama
5. Je ni kwa kiwango gani unawajali wengine ili nao waweze kukujali wewe
--Kujipenda kazi , ni zaidi ya kula bata !
Tafakari zetu

2013

Tafakari yetu leo:
Wewe ndie unayejifahamu zaidi kuliko mtu mwingine yeyote yule. Kumbuka hili hasa
unapohisi kukatishwa tamaa na maneno ya wengine.
Hao wanasema maoni yao, kutokana na waliyokumbana nayo, au waliyosikia,
waliyoyaona n.k, hata hivyo wewe ni wa pekee, mazingira yako, uliyopitia, bahati
yako, na pengine hawajajua uwezo wako halisi upo vipi.
Na hata kama wapo sahihi, bado ukweli ni kuwa unayo nafasi ya kubadilika, na
kuwaonyesha HAWAPO SAHIHI !
Wewe una nguvu sana,kuliko ulivyodhani, itumie nguvu yako.
--Siku njema fans.
Tafakari Yetu leo:
Jiulize kwanini wewe unadhani HAUWEZI kufanya mambo makubwa ya kijamii na
kimaendeleo ? Sio lazima kuwa maarufu ila kufanya jambo lenye kugusa na
kuboresha maisha ? Je ni kwa sababu :1. Hauna MTAJI wa kutosha: DELL ilianzishwa kwa mtaji mdogo sana kama dola
1000 tuu !
2: Wewe sio Maarufu : Mark Zuckerberg alianzisha FB akiwa chuoni wala hajawa
maarufu kama sasa.
3: Miundo Mbinu mibovu: Kuna mwafrika mwenzetu yupo Angola ambapo
katengeneza printer kwa kutumia takataka za vifaa vya kielectroniki
4: Hauishi Ulaya: Mwanamke wa kwanza mwana mahesabu (Hypatria) alikuwa
Mwafrika na aliishi Afrika.
5: Hauna elimu ya kutosha kama digrii au Masters: Bill Gates hakuwa hata na
degree alipoanzisha kampuni ya kutengeneza software ya Microsoft.
---Kumbuka la msingi sio nini kimekutokea katika maisha yako, bali ni kwa namna
gani wewe unayachukulia hayo yaliyokutokea. Dunia ni kama kisima kuna kila fursa,
ni wewe tuu jinsi ya kuchota. Je unashindaje mazingira au umekubali mazingira
yakushinde?
Tafakari yetu leo:
Kama una jambo la msingi la kufanya usiache kulifanya kwa kuogopa UTAKOSEA.
Utakosea tuu katika maisha yako, na hata usipofanya hilo unalotaka kufanya vado
watu watatafuta na kuweka wazi makosa (mapungufu) yako mengine.
Makosa yapo kila siku, utastaajabu kujua kuwa kwa wengine hata wewe kuwa hai au
kuwa hivyo na hapo ulipo wanaona ni kosa kubwa. Wanatamani ingekuwa
vinginevyo kabisa.
Tafakari zetu

2013

Tafakari yetu leo:
Wala usishangae mtu aliyekuwa tajiri kwa miaka 20, leo hii akafirisika na kuwa
maskini, wakati yule maskini mlalahoi aliyehangaika na kuishi katika ufukara kwa
miaka 30 leo hii akawa tajiri.
Maisha ni safari , maisha ni muda, thamini na mpe heshima yake kila mtu.
Tafakari Yetu Leo:
Ni kweli kuwa tunahitaji watu wa aina tofauti na fani tofauti, hata hivyo SIO LAZIMA
wewe ndio uwe wa kufanya kazi zisizolipa au usiyoipenda. Uchaguzi na Nguvu ni
Yako Kubadilika.
Tafakari Yetu Leo:
Fanya bidii katika mambo ya msingi kwa maisha yako, lakini usiache pia kuwa na
SUBIRA. Kwani kuna wakati, hata juhudi za kipekee haziwezi kuleta utakacho, bali
inakupasa usubiri wakati muafaka.
Tafakari Yetu Leo:
Unahisi Umekosea jambo, au Unaogopa Kujaribu utakosea? Msikie Eistein:Anyone who has never made a mistake has never tried anything new.- Eistein.
“Yeyote ambaye hajawahi kukosea basi hajawahi kujaribu jambo”
Fans, ijumaa njema na wikiend njema.
Wakati Tajiri anapomdhulumu maskini inaitwa Biashara, ila Masikini anapojaribu
kuzuia asidhulumiwe/anapodai haki yake, huwa inaitwa Kuwa na Vurugu.
Tafakari Yetu Leo:
Eti unaogopa kutia hasara au kukosea mbele za watu ? Wakati hata kuwa kwako hai
ni KOSA au hasara kwa wengine (Wanaokuchukia). La msingi katika maisha fanya
jambo linaloleta tija, usiogope watu, wala kukosea
Tafakari Yetu Leo:
Vitabu vya dini vinasisitiza tuelimike,na haviweki kikomo cha kuelimika. Je,
unajielimisha mara kwa mara? Unaitafuta elimu au unatafuta cheti/vyeti na vyeo tu?
Tafakari Yetu Leo:
MAISHA MAGUMU, SO WHAT ? Tuendelee Kulalamika na Kulaumu Wengine, Au
Tujibidiishe Katika Kufanya Kazi na Kupata Ufahamu wa Kutukomboa na Hali Hii ?.
Tafakari zetu
Tafakari Yetu Leo:
Ukitaka kukumbuka jambo vema, lielewe kwa ufasaha.
Ukitaka kuelewa kwa ufasaha, sikiliza au soma kwa umakini.
Ukitaka kuwa na umakini, jenga hamasa katika jambo husika.

2013

Contenu connexe

En vedette

2024 State of Marketing Report – by Hubspot
2024 State of Marketing Report – by Hubspot2024 State of Marketing Report – by Hubspot
2024 State of Marketing Report – by HubspotMarius Sescu
 
Everything You Need To Know About ChatGPT
Everything You Need To Know About ChatGPTEverything You Need To Know About ChatGPT
Everything You Need To Know About ChatGPTExpeed Software
 
Product Design Trends in 2024 | Teenage Engineerings
Product Design Trends in 2024 | Teenage EngineeringsProduct Design Trends in 2024 | Teenage Engineerings
Product Design Trends in 2024 | Teenage EngineeringsPixeldarts
 
How Race, Age and Gender Shape Attitudes Towards Mental Health
How Race, Age and Gender Shape Attitudes Towards Mental HealthHow Race, Age and Gender Shape Attitudes Towards Mental Health
How Race, Age and Gender Shape Attitudes Towards Mental HealthThinkNow
 
AI Trends in Creative Operations 2024 by Artwork Flow.pdf
AI Trends in Creative Operations 2024 by Artwork Flow.pdfAI Trends in Creative Operations 2024 by Artwork Flow.pdf
AI Trends in Creative Operations 2024 by Artwork Flow.pdfmarketingartwork
 
PEPSICO Presentation to CAGNY Conference Feb 2024
PEPSICO Presentation to CAGNY Conference Feb 2024PEPSICO Presentation to CAGNY Conference Feb 2024
PEPSICO Presentation to CAGNY Conference Feb 2024Neil Kimberley
 
Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)
Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)
Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)contently
 
How to Prepare For a Successful Job Search for 2024
How to Prepare For a Successful Job Search for 2024How to Prepare For a Successful Job Search for 2024
How to Prepare For a Successful Job Search for 2024Albert Qian
 
Social Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie Insights
Social Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie InsightsSocial Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie Insights
Social Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie InsightsKurio // The Social Media Age(ncy)
 
Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024
Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024
Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024Search Engine Journal
 
5 Public speaking tips from TED - Visualized summary
5 Public speaking tips from TED - Visualized summary5 Public speaking tips from TED - Visualized summary
5 Public speaking tips from TED - Visualized summarySpeakerHub
 
ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd
ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd
ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd Clark Boyd
 
Getting into the tech field. what next
Getting into the tech field. what next Getting into the tech field. what next
Getting into the tech field. what next Tessa Mero
 
Google's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search Intent
Google's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search IntentGoogle's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search Intent
Google's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search IntentLily Ray
 
Time Management & Productivity - Best Practices
Time Management & Productivity -  Best PracticesTime Management & Productivity -  Best Practices
Time Management & Productivity - Best PracticesVit Horky
 
The six step guide to practical project management
The six step guide to practical project managementThe six step guide to practical project management
The six step guide to practical project managementMindGenius
 
Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...
Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...
Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...RachelPearson36
 

En vedette (20)

2024 State of Marketing Report – by Hubspot
2024 State of Marketing Report – by Hubspot2024 State of Marketing Report – by Hubspot
2024 State of Marketing Report – by Hubspot
 
Everything You Need To Know About ChatGPT
Everything You Need To Know About ChatGPTEverything You Need To Know About ChatGPT
Everything You Need To Know About ChatGPT
 
Product Design Trends in 2024 | Teenage Engineerings
Product Design Trends in 2024 | Teenage EngineeringsProduct Design Trends in 2024 | Teenage Engineerings
Product Design Trends in 2024 | Teenage Engineerings
 
How Race, Age and Gender Shape Attitudes Towards Mental Health
How Race, Age and Gender Shape Attitudes Towards Mental HealthHow Race, Age and Gender Shape Attitudes Towards Mental Health
How Race, Age and Gender Shape Attitudes Towards Mental Health
 
AI Trends in Creative Operations 2024 by Artwork Flow.pdf
AI Trends in Creative Operations 2024 by Artwork Flow.pdfAI Trends in Creative Operations 2024 by Artwork Flow.pdf
AI Trends in Creative Operations 2024 by Artwork Flow.pdf
 
Skeleton Culture Code
Skeleton Culture CodeSkeleton Culture Code
Skeleton Culture Code
 
PEPSICO Presentation to CAGNY Conference Feb 2024
PEPSICO Presentation to CAGNY Conference Feb 2024PEPSICO Presentation to CAGNY Conference Feb 2024
PEPSICO Presentation to CAGNY Conference Feb 2024
 
Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)
Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)
Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)
 
How to Prepare For a Successful Job Search for 2024
How to Prepare For a Successful Job Search for 2024How to Prepare For a Successful Job Search for 2024
How to Prepare For a Successful Job Search for 2024
 
Social Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie Insights
Social Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie InsightsSocial Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie Insights
Social Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie Insights
 
Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024
Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024
Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024
 
5 Public speaking tips from TED - Visualized summary
5 Public speaking tips from TED - Visualized summary5 Public speaking tips from TED - Visualized summary
5 Public speaking tips from TED - Visualized summary
 
ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd
ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd
ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd
 
Getting into the tech field. what next
Getting into the tech field. what next Getting into the tech field. what next
Getting into the tech field. what next
 
Google's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search Intent
Google's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search IntentGoogle's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search Intent
Google's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search Intent
 
How to have difficult conversations
How to have difficult conversations How to have difficult conversations
How to have difficult conversations
 
Introduction to Data Science
Introduction to Data ScienceIntroduction to Data Science
Introduction to Data Science
 
Time Management & Productivity - Best Practices
Time Management & Productivity -  Best PracticesTime Management & Productivity -  Best Practices
Time Management & Productivity - Best Practices
 
The six step guide to practical project management
The six step guide to practical project managementThe six step guide to practical project management
The six step guide to practical project management
 
Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...
Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...
Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...
 

Tafakari mbuketimes

  • 2. Tafakari zetu 2013 Tafakari yetu leo: Inawezekana Suluhu ipo karibu sana ila tatizo wewe unafikiria upande mmoja tuu! --Jifunze toka ktk hadithi hii fupi: Mmama mmoja aliyekuwa akioga alitoka mkuku bafuni baada ya kusikia sauti ya picha ya X, toka chumbani kwa watoto wake. Kufika kweli watoto wake wenye umri wa miaka 6-10 walikuwa wakiangalia picha. Yeye kwa haraka akatoa khanga aliyokuwa amejifunga na kuifunika TV, yeye akabaki mtupu huku akiwakemea watoto. Mara baba naye aliyekuwa anajiandaa kuvaa chumbani akakurupuka akiwa kajifunga taulo tuu, kufika chumbani kwa watoto akaanza kumkaripia mkewe kuwa si vizuri kukaa mtupu mbele ya watoto hivyo akavua taulo na kumfunika mkewe, huku akimlaumu. --Ndio hivyo kuna nyakati waweza kujikuta unadhani suluhu ni moja tuu, kumbe ukifikiria zaidi waweza pata njia nyingi ya kupata suluhu ya magumu unayokumbana nayo. Fikiri kabla ya kufanya maamuzi hususani maamuzi mazito kama Mapenzi,Fedha,ajira, malezi ya watoto n.k Tafakari Yetu leo: Umekwisha sikia mara nyingi watu wakisema " Aaah mtu ukishamfahamu, hakupi shida". -- Leo nakutaka utumie msemo huo kwako mwenyewe yaani jiambie " Nikishajifahamu sintojipa shida". Kisha anza juhudi za kujifahamu kweli kweli, fanya bidii kukumbuka kwa kila wakati na tukio husika jinsi kujifahamu kwako kunavyoweza kusaidia au kutokukusaidia katika kutimiza majukumu yako ya msingi. Mfano: Unajifahamu vipi kuhusu matumizi ya fedha ?-basi ukiwa na mshahara au pato lolote kuwa makini Unajifahamu vipi kuhusu mapenzi -wivu na kujali? -basi kuwa makini Unajifahamu vipi kuhusu kujifunza mambo mapya ? -Badilisha hali isiyokusaidia kama vile kutokupenda kusoma. --Usijipe shida, JIFAHAMU, chukua hatua kurekebisha yasiyokusaidia. Tafakari yetu leo: Ukiwa darasani haileti maana kunyoosha mkono ili kujibu swali wakati haujui jibu. Mwalimu akikuchagua ukasimama na kusema haujui jibu, ni kujidhalilisha. Iweje leo unatafuta kazi wakati hauna ujuzi ulichosomea zaidi ya cheti tuu? Iweje unatafuta schorlaship wakati matokeo yao shule iliyopita ni ya kuunga unga, hata lugha mama ya elimu-english inakupiga chenga. Epuka mawazo ya kila kitu utaweza kwa kuunga unga. Jiwezeshe kuwa bora ktk mambo ya msingi.
  • 3. Tafakari zetu 2013 Tafakari yetu leo: Wanasema wanawake TISA hawawezi kushirikiana kubeba ujauzito ili kujifungua mtoto ndani ya MWEZI MMOJA. ---Sio kila ushirikiano unaoutafuta utakuletea mafanikio. Ushirikiano mwingine (team work) waweza rudisha nyuma maendeleo au isilete matarajio kabisa. Jifunze wakati fulani kufanya mambo wewe mwenyewe kwa ufanisi zaidi. Tafakari yetu: Kila kukicha dunia inabadilika, fursa na hatari zinaongezeka. Ni mbaya kama uwezo wako wa ufahamu haubadiliki. Mfano ajira haitegemei tena aina gani ya elimu uliyonayo bali uwezo na utayari wako wa kufanya kazi fulani. Lugha za kigeni na kompyuta hazihitajiki tena kuwa tuu kwenye cheti chako bali ni nyenzo haswa za 'kukutoa'. --Huu si muda wa kungoja kutafutwa, bali wewe mwenyewe chukua hatua ya kujiweka mbele ili uonekane. --Kila mtu sasa ni mzalishaji au mteja wako mtarajiwa, angalia unavyoonekana mbele ya wazalishaji wenzako na wateja wako watarajiwa. Muonekano wako na ufahamu wako utatumika kukuhukumu ktk kukupatia 'dili' na kufungua njia ya mafanikio yako. Tafakari yetu ni kuwa: Hauhitaji kujirusha toka ghorofa ya 20 kujua kama unaweza kufa kwa kufanya hivyo. ---Hivyo usiwe mgumu kuchukua tahadhali kuhusu ukimwi kwakuwa bado haujakukuta. Tafakari yetu leo: Fanya likupasalo kwa nguvu zako zote na maarifa yako yote bila kuhofu ni kwa kiwango gani ufanyacho kitaonekana BORA, kwani ubora wa jambo hautegemei tuu ufanyacho- mara nyingi hutegemea tafsiri za watu, muda uliopo, vitu vingine vilivyopo, taarifa ambazo watu wanazo, na zaidi sana uwepo wa watu wengine wafanyao kitu kama chako. --Inasikitisha watu hawajadili ubora wa kitu au mtu kwa kuangalia kitu au mtu mwenyewe bali mambo mengi kama hayo ndio maana leo simu za mche wa sabuni si mali tena, Messi ni bora zaidi ya Ronaldo, na hatari hata kwa wapenzi wanafananishwa na waliopita au watu tuu wengine huko mitaani. Hata MBUKE TIMES ni mbaya, ukilinganisha na blog nyingine uifikiriayo ni bora!
  • 4. Tafakari zetu 2013 Tafakari yetu leo ni: Ukiota ndoto nzuri unatamani iwe kweli, na hautamani iwe kweli -usingizini, bali unatamani iwe kweli katika maisha yako halisi-wakati umekwisha amka. ---Ndivyo ilivyo, kama unawaza na kutamani mambo mazuri katika maisha yako acha kuendelea kulala kijuhudi, kimawazo, kimbinu, na kimazingira. Mambo yanabadilika kila siku, amka sasa uanze kutekeleza unayotamani. Maneno matupu, mipango mitupu bila utekelezaji ni sawa na kuendelea kulala ukiota ndoto nzuri ambayo haikusaidii chochote huko usingizini hata kama ndoto hiyo inasema umekwa bilionea namba 1 dunia nzima. Tafakari yetu leo ni : Usikubali Teknolojia ichukue nafasi ya ubinadamu wako kwa kujiaminisha kuwa unaweza kuishi maisha ya namna mbili-moja ya hapa mtandaoni (FB) kwa lugha mbovu, ukajipa majina yasiyo yako, na kuandika "utakavyo" na nyingine eti wewe ni mtu mstaarabu na mwenye muelekeo wa maisha , mtu wa kutegemewa. --Labda tuu uwe na mkakati madhubuti katika kufanya hivyo, ila kujipa maisha yasiyo yako hapa mtandaoni kuna madhara mengi kwako kuliko faida zake. Unachoandika(kusema) ndicho kilichomo akilini mwako, na kilichomo akilini ndicho kinachokufanya uwe hivyo ulivyo, na ndivyo watu watakavyokuelewa. Tafakari yetu leo: Kigumu zaidi katika kujiletea mabadiliko sio ugumu wa kutenda unayopaswa kufanya ili kuleta mabadiliko bali ni Ugumu wa wewe kukubali kuwa mabadiliko yanawezekana, na kwamba wewe unaweza kubadilika. --Busara inaanza na kuweza kuji-amrisha kufanya tofauti na uliyokwishazoea,kuishinda hofu,na kufuta mengi uliyokwisha jifunza. JISHINDE WEWE MWENYEWE. Tafakari Yetu leo: Ukiacha familia gani umezaliwa, au nchi gani umezaliwa na uwepo wa bahati hapa na pale, chunguza kwa makini utagundua kushindwa kwako katika mambo mengi ni kwa sababu yako wewe mwenyewe ! --Hata hivyo una haki ya kushinda, unaweza kubadilika sasa na kuishi maisha ya ushindi. Fikiria kwa mapana, anza hata ikibidi kidogo kidogo kujiletea mabadiliko.
  • 5. Tafakari zetu 2013 Tafakari yetu leo: MAMBO YASIPOENDA SAWA LEO,KUMBUKA IPO KESHO PIA! Kuna utofauti mkubwa kati ya KUTUMAINI na KUTARAJIA kufanyika kwa jambo fulani. 1. Kutumaini kunakuruhusu kufikiria njia mbadala na kuwa na subira bali kutarajia ni kuwa na mtazamo wa aina moja na kutojiandaa au kutokuwa tayari kuchagua au kutafakari njia mbadala. 2.Kutumaini mara nyingi hakuleti maumivu makali kulinganisha na KUTARAJIA hususani pale mambo yanapoenda sivyo ndivyo. Mfano UNATUMAINI mtu atafanya kitu fulani ukimpatia kitu fulani, asipofanya sio shida sana, kuliko UKITARAJIA kabisa kuwa atafanya halafu asifanye,utabaki UNAHUZUNIKA. Tafakari yetu leo: Ingawa bahati ipo na pia tunafanya maombi lakini kumbuka maandalizi na juhudi ya kile unachotamani ni ya msingi, na pengine maandalizi na juhudi zako zinaweza kuwa SUMAKU ya BAHATI. --Chukulia mfano una kiingereza cha "kuokoteza" halafu unapata ufadhili wa kusoma UINGEREZA, ila kwanza unatakiwa ufanye interview ya ana kwa ana masaa mawili na timu ya wafadhili wako ! Utajikuta hivi hivi unaiacha bahati ! Tafakari yetu leo: Kumbuka ili kufanikiwa sio lazima ufanye kitu KIKUBWA au kwa USTADI mkubwa sana bali la msingi ni kufanya toka moyoni na kwa juhudi ya kiwango chako cha juu kabisa. --Biashara nyingi kubwa hazikuanza zikiwa kubwa, kuna makosa mengi mengi yalifanyika kabla ndege ya kwanza haijaanza kuruka hewani, kuna hasara nyingi katika ugunduzi mbalimbali kama baruti (niliandika hapa MBUKE TIMES) hata hivyo uduni wa mwanzo wa hayo ni historia tuu, hakuna anayetilia maanani. -Au basi embu jikumbushe SIMU za mkononi zilipotoka,enzi za "mche wa sabuni"mpaka Iphone. --Anza sasa kujishughulisha kwa ajili ya ndoto yako. Tafakari yetu: Mambo yafuatayo yanaweza onekana kama msaada katika kuleta furaha kwetu, hata hivyo kwa baadhi imekuwa kinyume,yanaongeza GHARAMA ya kuwa na FURAHA: 1. Utajiri 2. Marafiki wenye mafanikio 3. Mpenzi /Mke Mzuri 4. Ajira 5.Watoto --Zaidi ya kutafuta vitu tunavyodhani vitatupatia furaha tutumie muda pia kuboresha
  • 6. Tafakari zetu 2013 UFAHAMU wetu, tujitambue na tufanye akili zetu ziwe huru. Na zaidi sana TUMCHE MUNGU. Tafakari yetu leo: Watoto wanapoanza kujifunza kusoma huanza na A E I O U. Hata hesabu huanzia kuhesabu 1, 2, n.k. Hata hivyo leo hii wewe uliyeanza na A E I O U, unachat FB,kama vile sio yule ambaye A E I O U zilikuwa zinamsumbua ! --Mambo mazuri na makubwa huanza kidogo kidogo -Tukumbushane kaugonjwa ka kushindwa kuchukua hatua ya kuanza jambo la msingi! Hatua shuleni, makazini, katika mahusiano, biashara , n.k. --Kama hamasa umeshapata sana, kama masomo na mbinu hizo ulizonazo unaweza anza nazo kufanya jambo la msingi. Hata hivyo wengi tunasubiri mpaka tuwe na uwezo wa kufanya "jambo kubwa". Usingoje "uwezo mkubwa", anza kidogo kidogo, uzoefu utakaoupata na makosa utakayofanya yatakusaidia kujiweka vema hapo baadae. Tafakari yetu leo ni: "Usiogope kihivyo kuwa dunia itaisha leo hii Jumatano, kumbuka kuna nchi nyingine Jumatano yako kwao bado ni Jumanne, au ndio Alhamis yao " --- La msingi katika tafakari hii ni kuwa ingawa woga ni muhimu wakati fulani, ila angalia pia na vitu vya kuogopa! Vitu vingine unaogopa ni kwakuwa tuu hauna taarifa sahihi ! Tafakari yetu leo: Kirahisi rahisi huwa tunawaambia wengine tunawapenda na tupo tayari kufanya lolote kwa ajili yao. Tugeuze kibao sasa… Inaweza kuonekana kama jambo rahisi rahisi hivi, ila embu fikiria WEWE UNAJIPENDA KWELI KWELI . 1. Je ni kwa kiwango gani unajali afya yako: Ili uweze kuwepo kwa miaka mingi zaidi 2. Je ni kwa kiwango gani una juhudi ya kutafuta mambo ya kuboresha ufahamu wako, kupata busara zaidi ili uongeze nafasi za kuwa na furaha ( Kwa kuwa FURAHA kwa kiwango kikubwa ni vile tunavyochukulia mambo –kifikra zetu na fikra zetu zinaboreshwa au kudhoofishwa na kiwango cha ufahamu, uzoefu na makuzi yetu) 3. Je ni kwa kiwango gani una juhudi katika kufanya bidii ya kazi ya kukupatia kipato , au una zuga zuga tuu ugange njaa 4. Je ni kwa kiwango gani unafanya mazingira uliyopo yawe masafi na salama ili wewe ubaki kuwa salama 5. Je ni kwa kiwango gani unawajali wengine ili nao waweze kukujali wewe --Kujipenda kazi , ni zaidi ya kula bata !
  • 7. Tafakari zetu 2013 Tafakari yetu leo: Wewe ndie unayejifahamu zaidi kuliko mtu mwingine yeyote yule. Kumbuka hili hasa unapohisi kukatishwa tamaa na maneno ya wengine. Hao wanasema maoni yao, kutokana na waliyokumbana nayo, au waliyosikia, waliyoyaona n.k, hata hivyo wewe ni wa pekee, mazingira yako, uliyopitia, bahati yako, na pengine hawajajua uwezo wako halisi upo vipi. Na hata kama wapo sahihi, bado ukweli ni kuwa unayo nafasi ya kubadilika, na kuwaonyesha HAWAPO SAHIHI ! Wewe una nguvu sana,kuliko ulivyodhani, itumie nguvu yako. --Siku njema fans. Tafakari Yetu leo: Jiulize kwanini wewe unadhani HAUWEZI kufanya mambo makubwa ya kijamii na kimaendeleo ? Sio lazima kuwa maarufu ila kufanya jambo lenye kugusa na kuboresha maisha ? Je ni kwa sababu :1. Hauna MTAJI wa kutosha: DELL ilianzishwa kwa mtaji mdogo sana kama dola 1000 tuu ! 2: Wewe sio Maarufu : Mark Zuckerberg alianzisha FB akiwa chuoni wala hajawa maarufu kama sasa. 3: Miundo Mbinu mibovu: Kuna mwafrika mwenzetu yupo Angola ambapo katengeneza printer kwa kutumia takataka za vifaa vya kielectroniki 4: Hauishi Ulaya: Mwanamke wa kwanza mwana mahesabu (Hypatria) alikuwa Mwafrika na aliishi Afrika. 5: Hauna elimu ya kutosha kama digrii au Masters: Bill Gates hakuwa hata na degree alipoanzisha kampuni ya kutengeneza software ya Microsoft. ---Kumbuka la msingi sio nini kimekutokea katika maisha yako, bali ni kwa namna gani wewe unayachukulia hayo yaliyokutokea. Dunia ni kama kisima kuna kila fursa, ni wewe tuu jinsi ya kuchota. Je unashindaje mazingira au umekubali mazingira yakushinde? Tafakari yetu leo: Kama una jambo la msingi la kufanya usiache kulifanya kwa kuogopa UTAKOSEA. Utakosea tuu katika maisha yako, na hata usipofanya hilo unalotaka kufanya vado watu watatafuta na kuweka wazi makosa (mapungufu) yako mengine. Makosa yapo kila siku, utastaajabu kujua kuwa kwa wengine hata wewe kuwa hai au kuwa hivyo na hapo ulipo wanaona ni kosa kubwa. Wanatamani ingekuwa vinginevyo kabisa.
  • 8. Tafakari zetu 2013 Tafakari yetu leo: Wala usishangae mtu aliyekuwa tajiri kwa miaka 20, leo hii akafirisika na kuwa maskini, wakati yule maskini mlalahoi aliyehangaika na kuishi katika ufukara kwa miaka 30 leo hii akawa tajiri. Maisha ni safari , maisha ni muda, thamini na mpe heshima yake kila mtu. Tafakari Yetu Leo: Ni kweli kuwa tunahitaji watu wa aina tofauti na fani tofauti, hata hivyo SIO LAZIMA wewe ndio uwe wa kufanya kazi zisizolipa au usiyoipenda. Uchaguzi na Nguvu ni Yako Kubadilika. Tafakari Yetu Leo: Fanya bidii katika mambo ya msingi kwa maisha yako, lakini usiache pia kuwa na SUBIRA. Kwani kuna wakati, hata juhudi za kipekee haziwezi kuleta utakacho, bali inakupasa usubiri wakati muafaka. Tafakari Yetu Leo: Unahisi Umekosea jambo, au Unaogopa Kujaribu utakosea? Msikie Eistein:Anyone who has never made a mistake has never tried anything new.- Eistein. “Yeyote ambaye hajawahi kukosea basi hajawahi kujaribu jambo” Fans, ijumaa njema na wikiend njema. Wakati Tajiri anapomdhulumu maskini inaitwa Biashara, ila Masikini anapojaribu kuzuia asidhulumiwe/anapodai haki yake, huwa inaitwa Kuwa na Vurugu. Tafakari Yetu Leo: Eti unaogopa kutia hasara au kukosea mbele za watu ? Wakati hata kuwa kwako hai ni KOSA au hasara kwa wengine (Wanaokuchukia). La msingi katika maisha fanya jambo linaloleta tija, usiogope watu, wala kukosea Tafakari Yetu Leo: Vitabu vya dini vinasisitiza tuelimike,na haviweki kikomo cha kuelimika. Je, unajielimisha mara kwa mara? Unaitafuta elimu au unatafuta cheti/vyeti na vyeo tu? Tafakari Yetu Leo: MAISHA MAGUMU, SO WHAT ? Tuendelee Kulalamika na Kulaumu Wengine, Au Tujibidiishe Katika Kufanya Kazi na Kupata Ufahamu wa Kutukomboa na Hali Hii ?.
  • 9. Tafakari zetu Tafakari Yetu Leo: Ukitaka kukumbuka jambo vema, lielewe kwa ufasaha. Ukitaka kuelewa kwa ufasaha, sikiliza au soma kwa umakini. Ukitaka kuwa na umakini, jenga hamasa katika jambo husika. 2013