SlideShare une entreprise Scribd logo
1  sur  5
Télécharger pour lire hors ligne
KILIMO BORA CHA NYANYA
MAGONJWA NA WADUDU
Utangulizi
Nyanya ni zao la chakula na biashara. Kilimo cha zao hili hufanyika majira yote
(masika na kiangazi), na faida hupatikana haraka na ni ya kuridhisha ikilinganishwa
na mazao mengine. Pamoja na umuhimu wa zao hili, wadudu waharibifu na
magonjwa huathiri uzalishaji na ubora wa matunda. Ili mkulima aweze kupata faida
na kuongeza pato la kaya yake ni vema kuzingatia udhibiti wa magonjwa na wadudu
wa zao hili. Kipeperushi hiki kinatoa maelezo ya udhibiti wa magonjwa na wadudu
muhimu ya zao la Nyanya.
MAGONJWA YA NYANYA
Bakajani chelewa (Late blight)
Ugonjwa huu huenenzwa na vimelea vya fangasi. Husababishwa na hali ya hewa hasa
ya unyevunyevu, na huenezwa na upepo. Majani, shina, matunda hushambuliwa.
Majani huwa na ukungu mweupe na kijivu, na baadaye hukauka. Matunda huwa na
mabaka ya kikahawia na baadaye kuoza. Mashina pia huwa na mabaka ya kikahawia.
Udhibiti
• Nyunyiza dawa ya kuzuia ukungu hasa wakati wa masika, Dawa
zinazopendekezwa ni Ridomil, Dithane 45, Bravo, Funguran, milraz.
• Fanya mzunguko wa mazao. Usipande nyanya sehemu moja kila msimu au
palipolimwa mazao jamii ya nyanya km viazi mviringo, bilinganya, aina zote
za pilipili na nyanya chungu.
• Tumia mbegu safi
• Panda aina za nyanya zinazovumilia ugomjwa
Bakajani tangulia (Early blight)
Huenezwa na vimelea vya fangasi. Husababishwa na kuenezwa na hali ya hewa
pamoja na mbegu zenye ugonjwa. Mabaka ya kahawia yenye mistari ya mviringo
huonekana kwenye majani na shina. Baka jeusi hutokea sehemu ya tunda
inayoshikana na kikonyo.
Udhibiti
• Nyunyiza dawa ya Kocide, Funguran
• Teketeza mabaka ya mazao baada ya kuvuna
• Tumia mbegu safi na bora
Mnyauko fusari (Fusarium wilt)
Huenezwa na mbegu zenye ugonjwa. Husambazwa na vimelea vya fungasi
vinavyoishi kwenye udongo.
Ugonjwa hujitokeza zaidi wakati wa kiangazi. Vimelea hushambulia sehemu au
mirija ya mmea ya kupitishia maji na chakula. Mmea hukosa maji na chakula na
hatimaye hunyauka. Shina la mmea likipasuliwa ndani huonekana rangi ya kikahawia.
Udhibiti
• Tumia mbegu safi na bora
• Tumia mzunguko wa mazao. Nyanya zisizungushwe na mazao jamii yake
• Teketeza masalia ya mimea
• Choma kitalu cha nyanya kabla ya kusia mbegu
Mnyauko bacteria (Bacterial wilt)
Ugonjwa husababishwa na vimelea vya bacteria vinavyoishi kwenye udongo.
Huenezwa na kusambazwa na mbegu na udongo wenye vimelea. Mirija ya mimea ya
kupitishia maji na chakula hushambulia na mimea hunyauka ghafla. Mmea hukauka
na kufa.
Udhibiti
• Panda mbegu safi
• Panda nyanya sehemu ambayo haijawahi kupandwa viazi mviringo,
bilinganya au nyanya chungu
• Tumia mzunguko wa mazao
• Hakikisha mfereji wa maji ya kumwagilia hayapiti kwenye shamba lenye
historia ya ugonjwa huu.
• Choma kitalu cha nyanya kabla ya kusia mbegu
Mnyauko vetisili (Verticillum wilt)
Hakuna dawa inayozuia au kutibu ugonjwa huu kwa sasa. Ugonjwa husababishwa na
ukungu (fangasi) kwenye udongo. Ukungu huu huishi kwenye udongo kwa muda
mrefu bila kudhurika. Ugonjwa huongezeka ikiwa mizimizi ya nyanya
imeshambuliwa na minyo fundo; au kukiwepo na hali ya ubaridi au ukame. Ugonjwa
husababisha hasara kubwa. Ugonjwa hushambulia sehemu ya ndani ya shina na
kusababisha sehemu hiyo kuwa na rangi ya kijivu. Majani hugeuka njano na mimea
kunyauka na kufa.
Udhibiti
• Tumia mzunguko wa mazao usiopungua miaka mine
• Ondoa mabaki ya nyanya shambani
• Tumia mbegu bora na safi
Bakadoa (Bacterial spot)
Ugonjwa huu huenezwa na vimelea vya bacteria vinavyoishi kwenye mbegu, pia
kwenye hewa. Huenezwa kwa kasi sana wakati wa masika. Madoa ya rangi kahawia
huonekana kwenye majani na matunda.
Udhibiti
• Panda mbegu bora na safi
• Tumia mzunguko wa mazao
• Teketeza masalia ya mazao
• Nyunyizia dawa ya funguran, Kocide101, Cobox, Bravo
Makovu bakteria (Bacterial canker)
Ugonjwa huenezwa na vimelea vya bacteria vinavyoishi kwenye mbegu na hewani.
Hutokea zaidi wakati wa masika. Majani hukauka nchani na makovu yaliyodidimia
hutokea kwenye shina. Matunda huwa na makovu yenye rangi ya kahawia sehemu ya
katikati.
Udhibiti
• Tumia mbegu bora na safi
• Teketeza masalia ya mazao
• Tumia mzunguko wa mazao
2
Rasta (Yellow leaf curl)
Ugonjwa huu husababishwa na virusi na huenezwa na nzi wadogo weupe. Hutokea
zaidi wakati wa kiangazi. Mimea hudumaa na majani yaliyoshambuliwa huwa na
rangi ya manjano na pengine rangi ya zambarau. Nyanya hupasuka.
Udhibiti
• Nyunyiza dawa za sumu za kuua wadudu (Selecron, Dursburn, Actelic)
• Ng’oa mimea yenye ugonjwa
• Tumia mzunguko wa mazao
• Weka shamba katika hali ya usafi
Batobato (Tomato mosaic virus)
Ugonjwa husababishwa na virusi na hueezwa na mbegu na kugusana. Majani huwa na
mchanganyiko wa rangi hasa kijani kibichi na kijani kilichofifia (majano). Majani
hujikunja na manjani machanga huwa na maumbile yasiyo kawaida. Ukifikisha jani
huwa linavinjikavunjika.
Udhibiti
• Tumia mbegu bora na safi
• Ng’oa mimea iliyoshambuliwa
• Teketeza masalia ya mazao
• Weka shamba katika hali ya usafi
WADUDU WAHARIBIFU
Viwavi Matunda (Fruit worm)
Viwavi hawa hutokana na wadudu nondo. Viwavi hutoboa matunda na kuacha
matundu na hatimaye matunda huoza. Hupunguza ubora wa matunda.
Udhibiti
Nyunyizia dawa ya kuua wadudu. Dawa hizo ni pamoja na Actelic 50EC, Selectron,
Dursbaan, Maji ya majani ya mwarobaini au utupa pia huua wadudu.
Utitiri wekundu (Red Spider mites)
Hawa ni wadudu wekundu, wadogo sana wanaoweka utando chini ya majani, hasa
wakati wa kiangazi. Wadudu hawa hufyonza utomvu kwenye majani na kusababisha
majani kukauka.
Udhibiti
• Nyunyizia dawa za sumu. Dawa hizo ni pamoja na Actellic, Selecron,
Dursbarn na Thionex
• Mwagilia maji mara kwa mara
• Weka shamba katika hali ya usafi
Inzi weupe (White flies)
Hawa ni Inzi weupe wadogo sana. Hujitokeza sana wakati wa kiangazi. Hueneza
ugonjwa wa virusi ujulikanao kama Rasta.
3
Udhibiti
Nyunyizia dawa za sumu za kuulia wadudu kama Selecron, Actellic, Dursban na
thionex. Pia maji ya majani ya mwarobaini na utupa.
Vidukari au Wadudu mafuta (Aphids)
Ni wadudu wenye rangi nyeusi au kuijani au kahawia. Hukaa chini ya majani na
kufyonza utomvu kwenye majani machanga. Hudumaza mmea na kushindwa kuzaa
matunda
Udhibiti
Nyunyizia dawa za sumu za kuulia wadudu kama Rogor, Actellic, Selecron, Dursban
maji ya majani ya mwarobaini na utupa, maji ya pilipili.
Minyoo (Nematodes)
Ni minyoo midogomidogo ambayo hushambulia mizizi na kuweka vifundo. Mizizi
hushindwa kuchukua maji na chakula kwenye udongo. Mimea hudumaa na
kushindwa kuzaa
Udhibiti
• Tumia mzunguko wa mazao
• Choma udongo wa kitalu kabla ya kusia mbegu kwa kutumia karatasi la
plastiki jeusi na nishati ya jua
• Choma masalia ya mazao
Sota (Cutworms)
Hushambulia miche ya nyanya hasa baada ya kupandikizwa shambani. Wakati wa
mchana hujificha kwenye udongo na usiku hujitokeza na kukata miche kwenye shina
usawa wa udongo.
Udhibiti
• Nyunyiza dawa za kuua wadudu kwenye shina usawa wa udongo
• Hakikisha miche inapata maji ya kutosha.
Kimetolewa na:
Taasisi ya Utafiti Kilimo Uyole,
Kitengo cha Mboga na Matunda
S.L.P.400
MBEYA, TANZANIA
Simu: 025 – 2510363
Fax: 025 – 2510065
E-mail: ariuyole@iwayafrica.com
4
5

Contenu connexe

Tendances

Avocado - a Short guide for Growing and Operational Procedures.pdf
Avocado - a Short guide for Growing and Operational Procedures.pdfAvocado - a Short guide for Growing and Operational Procedures.pdf
Avocado - a Short guide for Growing and Operational Procedures.pdfIan Carlo Bottinelli Wolleter
 
Preservation of mulberry leafs and shoots
Preservation of mulberry leafs and shootsPreservation of mulberry leafs and shoots
Preservation of mulberry leafs and shootsB S.N.S.Gowtham Kumar
 
Different types of housing of animals
Different types of housing of animalsDifferent types of housing of animals
Different types of housing of animalsRameswar Panda
 
INDIGENOUS AND EXOTIC BREEDS OF LIVESTOCK
INDIGENOUS AND EXOTIC BREEDS OF LIVESTOCKINDIGENOUS AND EXOTIC BREEDS OF LIVESTOCK
INDIGENOUS AND EXOTIC BREEDS OF LIVESTOCKShekhAlisha
 
Demographic distribution of livestock 1.pptx
Demographic distribution of livestock 1.pptxDemographic distribution of livestock 1.pptx
Demographic distribution of livestock 1.pptxtsvanil1
 
presentation on chickpea
presentation on chickpea presentation on chickpea
presentation on chickpea Sunil Bhardwaj
 
Basics of sugar technology
Basics of sugar technologyBasics of sugar technology
Basics of sugar technologyDuraisamy Ramesh
 
Postharvest Management of Banana
Postharvest Management of BananaPostharvest Management of Banana
Postharvest Management of BananaSamar Biswas
 
identify indigenous breed f sheep and goat.pptx
identify indigenous breed f sheep and goat.pptxidentify indigenous breed f sheep and goat.pptx
identify indigenous breed f sheep and goat.pptxmanojj123
 
Modifications in Insect leg
Modifications in Insect legModifications in Insect leg
Modifications in Insect legYuvraj Singh
 
Cassava leaf spot
Cassava leaf spotCassava leaf spot
Cassava leaf spotMoni Bala
 

Tendances (20)

Root and tuber crops.pptx vvu
Root and tuber crops.pptx vvuRoot and tuber crops.pptx vvu
Root and tuber crops.pptx vvu
 
Potato
PotatoPotato
Potato
 
Avocado - a Short guide for Growing and Operational Procedures.pdf
Avocado - a Short guide for Growing and Operational Procedures.pdfAvocado - a Short guide for Growing and Operational Procedures.pdf
Avocado - a Short guide for Growing and Operational Procedures.pdf
 
Preservation of mulberry leafs and shoots
Preservation of mulberry leafs and shootsPreservation of mulberry leafs and shoots
Preservation of mulberry leafs and shoots
 
Different types of housing of animals
Different types of housing of animalsDifferent types of housing of animals
Different types of housing of animals
 
Birds Management
Birds ManagementBirds Management
Birds Management
 
INDIGENOUS AND EXOTIC BREEDS OF LIVESTOCK
INDIGENOUS AND EXOTIC BREEDS OF LIVESTOCKINDIGENOUS AND EXOTIC BREEDS OF LIVESTOCK
INDIGENOUS AND EXOTIC BREEDS OF LIVESTOCK
 
Hay making
Hay makingHay making
Hay making
 
Demographic distribution of livestock 1.pptx
Demographic distribution of livestock 1.pptxDemographic distribution of livestock 1.pptx
Demographic distribution of livestock 1.pptx
 
Litchi ppt
Litchi pptLitchi ppt
Litchi ppt
 
presentation on chickpea
presentation on chickpea presentation on chickpea
presentation on chickpea
 
Basics of sugar technology
Basics of sugar technologyBasics of sugar technology
Basics of sugar technology
 
Postharvest Management of Banana
Postharvest Management of BananaPostharvest Management of Banana
Postharvest Management of Banana
 
Nematode biology
Nematode biology Nematode biology
Nematode biology
 
identify indigenous breed f sheep and goat.pptx
identify indigenous breed f sheep and goat.pptxidentify indigenous breed f sheep and goat.pptx
identify indigenous breed f sheep and goat.pptx
 
Methods of flaying
Methods of flayingMethods of flaying
Methods of flaying
 
Modifications in Insect leg
Modifications in Insect legModifications in Insect leg
Modifications in Insect leg
 
Pest of plantation crops
Pest of plantation cropsPest of plantation crops
Pest of plantation crops
 
Urban pest house fly-ssnaik tnau Ph.D Scholar
Urban pest house fly-ssnaik tnau Ph.D ScholarUrban pest house fly-ssnaik tnau Ph.D Scholar
Urban pest house fly-ssnaik tnau Ph.D Scholar
 
Cassava leaf spot
Cassava leaf spotCassava leaf spot
Cassava leaf spot
 

Plus de isidori masalu

Disease i dandmanagementa5swahili-16wslkh
Disease i dandmanagementa5swahili-16wslkhDisease i dandmanagementa5swahili-16wslkh
Disease i dandmanagementa5swahili-16wslkhisidori masalu
 
Microsoft wordkanunizaufugajiborawami
Microsoft wordkanunizaufugajiborawamiMicrosoft wordkanunizaufugajiborawami
Microsoft wordkanunizaufugajiborawamiisidori masalu
 
Ufugaji bora-wa-nguruwe
Ufugaji bora-wa-nguruweUfugaji bora-wa-nguruwe
Ufugaji bora-wa-nguruweisidori masalu
 
Chanjo na tiba ya magojwa
Chanjo na tiba ya magojwa Chanjo na tiba ya magojwa
Chanjo na tiba ya magojwa isidori masalu
 
Mboga mboga-vegetables
Mboga mboga-vegetablesMboga mboga-vegetables
Mboga mboga-vegetablesisidori masalu
 
Mwongozo uzalishaji mazao-crop_guideline-tanzania-04_july2017
Mwongozo uzalishaji mazao-crop_guideline-tanzania-04_july2017Mwongozo uzalishaji mazao-crop_guideline-tanzania-04_july2017
Mwongozo uzalishaji mazao-crop_guideline-tanzania-04_july2017isidori masalu
 
Livestock diseases post pn-392
Livestock diseases post pn-392Livestock diseases post pn-392
Livestock diseases post pn-392isidori masalu
 

Plus de isidori masalu (12)

PIGS PRODUCTION.pdf
PIGS PRODUCTION.pdfPIGS PRODUCTION.pdf
PIGS PRODUCTION.pdf
 
Disease i dandmanagementa5swahili-16wslkh
Disease i dandmanagementa5swahili-16wslkhDisease i dandmanagementa5swahili-16wslkh
Disease i dandmanagementa5swahili-16wslkh
 
Watermelon swa
Watermelon swa Watermelon swa
Watermelon swa
 
Bustani.pdf
Bustani.pdfBustani.pdf
Bustani.pdf
 
Microsoft wordkanunizaufugajiborawami
Microsoft wordkanunizaufugajiborawamiMicrosoft wordkanunizaufugajiborawami
Microsoft wordkanunizaufugajiborawami
 
Ufugaji bora-wa-nguruwe
Ufugaji bora-wa-nguruweUfugaji bora-wa-nguruwe
Ufugaji bora-wa-nguruwe
 
Chanjo na tiba ya magojwa
Chanjo na tiba ya magojwa Chanjo na tiba ya magojwa
Chanjo na tiba ya magojwa
 
Mpunga rice-swahili_
Mpunga  rice-swahili_Mpunga  rice-swahili_
Mpunga rice-swahili_
 
Mboga mboga-vegetables
Mboga mboga-vegetablesMboga mboga-vegetables
Mboga mboga-vegetables
 
Mwongozo uzalishaji mazao-crop_guideline-tanzania-04_july2017
Mwongozo uzalishaji mazao-crop_guideline-tanzania-04_july2017Mwongozo uzalishaji mazao-crop_guideline-tanzania-04_july2017
Mwongozo uzalishaji mazao-crop_guideline-tanzania-04_july2017
 
Livestock diseases post pn-392
Livestock diseases post pn-392Livestock diseases post pn-392
Livestock diseases post pn-392
 
Livestock diseases
Livestock diseasesLivestock diseases
Livestock diseases
 

Kilimo bora cha nyanya

  • 1. KILIMO BORA CHA NYANYA MAGONJWA NA WADUDU Utangulizi Nyanya ni zao la chakula na biashara. Kilimo cha zao hili hufanyika majira yote (masika na kiangazi), na faida hupatikana haraka na ni ya kuridhisha ikilinganishwa na mazao mengine. Pamoja na umuhimu wa zao hili, wadudu waharibifu na magonjwa huathiri uzalishaji na ubora wa matunda. Ili mkulima aweze kupata faida na kuongeza pato la kaya yake ni vema kuzingatia udhibiti wa magonjwa na wadudu wa zao hili. Kipeperushi hiki kinatoa maelezo ya udhibiti wa magonjwa na wadudu muhimu ya zao la Nyanya. MAGONJWA YA NYANYA Bakajani chelewa (Late blight) Ugonjwa huu huenenzwa na vimelea vya fangasi. Husababishwa na hali ya hewa hasa ya unyevunyevu, na huenezwa na upepo. Majani, shina, matunda hushambuliwa. Majani huwa na ukungu mweupe na kijivu, na baadaye hukauka. Matunda huwa na mabaka ya kikahawia na baadaye kuoza. Mashina pia huwa na mabaka ya kikahawia. Udhibiti • Nyunyiza dawa ya kuzuia ukungu hasa wakati wa masika, Dawa zinazopendekezwa ni Ridomil, Dithane 45, Bravo, Funguran, milraz. • Fanya mzunguko wa mazao. Usipande nyanya sehemu moja kila msimu au palipolimwa mazao jamii ya nyanya km viazi mviringo, bilinganya, aina zote za pilipili na nyanya chungu. • Tumia mbegu safi • Panda aina za nyanya zinazovumilia ugomjwa Bakajani tangulia (Early blight) Huenezwa na vimelea vya fangasi. Husababishwa na kuenezwa na hali ya hewa pamoja na mbegu zenye ugonjwa. Mabaka ya kahawia yenye mistari ya mviringo huonekana kwenye majani na shina. Baka jeusi hutokea sehemu ya tunda inayoshikana na kikonyo. Udhibiti • Nyunyiza dawa ya Kocide, Funguran • Teketeza mabaka ya mazao baada ya kuvuna • Tumia mbegu safi na bora Mnyauko fusari (Fusarium wilt) Huenezwa na mbegu zenye ugonjwa. Husambazwa na vimelea vya fungasi vinavyoishi kwenye udongo. Ugonjwa hujitokeza zaidi wakati wa kiangazi. Vimelea hushambulia sehemu au mirija ya mmea ya kupitishia maji na chakula. Mmea hukosa maji na chakula na hatimaye hunyauka. Shina la mmea likipasuliwa ndani huonekana rangi ya kikahawia. Udhibiti • Tumia mbegu safi na bora • Tumia mzunguko wa mazao. Nyanya zisizungushwe na mazao jamii yake • Teketeza masalia ya mimea • Choma kitalu cha nyanya kabla ya kusia mbegu
  • 2. Mnyauko bacteria (Bacterial wilt) Ugonjwa husababishwa na vimelea vya bacteria vinavyoishi kwenye udongo. Huenezwa na kusambazwa na mbegu na udongo wenye vimelea. Mirija ya mimea ya kupitishia maji na chakula hushambulia na mimea hunyauka ghafla. Mmea hukauka na kufa. Udhibiti • Panda mbegu safi • Panda nyanya sehemu ambayo haijawahi kupandwa viazi mviringo, bilinganya au nyanya chungu • Tumia mzunguko wa mazao • Hakikisha mfereji wa maji ya kumwagilia hayapiti kwenye shamba lenye historia ya ugonjwa huu. • Choma kitalu cha nyanya kabla ya kusia mbegu Mnyauko vetisili (Verticillum wilt) Hakuna dawa inayozuia au kutibu ugonjwa huu kwa sasa. Ugonjwa husababishwa na ukungu (fangasi) kwenye udongo. Ukungu huu huishi kwenye udongo kwa muda mrefu bila kudhurika. Ugonjwa huongezeka ikiwa mizimizi ya nyanya imeshambuliwa na minyo fundo; au kukiwepo na hali ya ubaridi au ukame. Ugonjwa husababisha hasara kubwa. Ugonjwa hushambulia sehemu ya ndani ya shina na kusababisha sehemu hiyo kuwa na rangi ya kijivu. Majani hugeuka njano na mimea kunyauka na kufa. Udhibiti • Tumia mzunguko wa mazao usiopungua miaka mine • Ondoa mabaki ya nyanya shambani • Tumia mbegu bora na safi Bakadoa (Bacterial spot) Ugonjwa huu huenezwa na vimelea vya bacteria vinavyoishi kwenye mbegu, pia kwenye hewa. Huenezwa kwa kasi sana wakati wa masika. Madoa ya rangi kahawia huonekana kwenye majani na matunda. Udhibiti • Panda mbegu bora na safi • Tumia mzunguko wa mazao • Teketeza masalia ya mazao • Nyunyizia dawa ya funguran, Kocide101, Cobox, Bravo Makovu bakteria (Bacterial canker) Ugonjwa huenezwa na vimelea vya bacteria vinavyoishi kwenye mbegu na hewani. Hutokea zaidi wakati wa masika. Majani hukauka nchani na makovu yaliyodidimia hutokea kwenye shina. Matunda huwa na makovu yenye rangi ya kahawia sehemu ya katikati. Udhibiti • Tumia mbegu bora na safi • Teketeza masalia ya mazao • Tumia mzunguko wa mazao 2
  • 3. Rasta (Yellow leaf curl) Ugonjwa huu husababishwa na virusi na huenezwa na nzi wadogo weupe. Hutokea zaidi wakati wa kiangazi. Mimea hudumaa na majani yaliyoshambuliwa huwa na rangi ya manjano na pengine rangi ya zambarau. Nyanya hupasuka. Udhibiti • Nyunyiza dawa za sumu za kuua wadudu (Selecron, Dursburn, Actelic) • Ng’oa mimea yenye ugonjwa • Tumia mzunguko wa mazao • Weka shamba katika hali ya usafi Batobato (Tomato mosaic virus) Ugonjwa husababishwa na virusi na hueezwa na mbegu na kugusana. Majani huwa na mchanganyiko wa rangi hasa kijani kibichi na kijani kilichofifia (majano). Majani hujikunja na manjani machanga huwa na maumbile yasiyo kawaida. Ukifikisha jani huwa linavinjikavunjika. Udhibiti • Tumia mbegu bora na safi • Ng’oa mimea iliyoshambuliwa • Teketeza masalia ya mazao • Weka shamba katika hali ya usafi WADUDU WAHARIBIFU Viwavi Matunda (Fruit worm) Viwavi hawa hutokana na wadudu nondo. Viwavi hutoboa matunda na kuacha matundu na hatimaye matunda huoza. Hupunguza ubora wa matunda. Udhibiti Nyunyizia dawa ya kuua wadudu. Dawa hizo ni pamoja na Actelic 50EC, Selectron, Dursbaan, Maji ya majani ya mwarobaini au utupa pia huua wadudu. Utitiri wekundu (Red Spider mites) Hawa ni wadudu wekundu, wadogo sana wanaoweka utando chini ya majani, hasa wakati wa kiangazi. Wadudu hawa hufyonza utomvu kwenye majani na kusababisha majani kukauka. Udhibiti • Nyunyizia dawa za sumu. Dawa hizo ni pamoja na Actellic, Selecron, Dursbarn na Thionex • Mwagilia maji mara kwa mara • Weka shamba katika hali ya usafi Inzi weupe (White flies) Hawa ni Inzi weupe wadogo sana. Hujitokeza sana wakati wa kiangazi. Hueneza ugonjwa wa virusi ujulikanao kama Rasta. 3
  • 4. Udhibiti Nyunyizia dawa za sumu za kuulia wadudu kama Selecron, Actellic, Dursban na thionex. Pia maji ya majani ya mwarobaini na utupa. Vidukari au Wadudu mafuta (Aphids) Ni wadudu wenye rangi nyeusi au kuijani au kahawia. Hukaa chini ya majani na kufyonza utomvu kwenye majani machanga. Hudumaza mmea na kushindwa kuzaa matunda Udhibiti Nyunyizia dawa za sumu za kuulia wadudu kama Rogor, Actellic, Selecron, Dursban maji ya majani ya mwarobaini na utupa, maji ya pilipili. Minyoo (Nematodes) Ni minyoo midogomidogo ambayo hushambulia mizizi na kuweka vifundo. Mizizi hushindwa kuchukua maji na chakula kwenye udongo. Mimea hudumaa na kushindwa kuzaa Udhibiti • Tumia mzunguko wa mazao • Choma udongo wa kitalu kabla ya kusia mbegu kwa kutumia karatasi la plastiki jeusi na nishati ya jua • Choma masalia ya mazao Sota (Cutworms) Hushambulia miche ya nyanya hasa baada ya kupandikizwa shambani. Wakati wa mchana hujificha kwenye udongo na usiku hujitokeza na kukata miche kwenye shina usawa wa udongo. Udhibiti • Nyunyiza dawa za kuua wadudu kwenye shina usawa wa udongo • Hakikisha miche inapata maji ya kutosha. Kimetolewa na: Taasisi ya Utafiti Kilimo Uyole, Kitengo cha Mboga na Matunda S.L.P.400 MBEYA, TANZANIA Simu: 025 – 2510363 Fax: 025 – 2510065 E-mail: ariuyole@iwayafrica.com 4
  • 5. 5